SW/Prabhupada 0009 - The Thief Who Became A Devotee

Revision as of 05:13, 12 July 2019 by Vanibot (talk | contribs) (Vanibot #0023: VideoLocalizer - changed YouTube player to show hard-coded subtitles version)
(diff) ← Older revision | Latest revision (diff) | Newer revision → (diff)


Lecture on SB 1.2.12 -- Los Angeles, August 15, 1972

Krishna anasema kwenye Bhagavad-gītā: (BG 7.25) nāhaṁ prakāśaḥ sarvasya yoga-māyā-samāvṛtaḥ "Sijithiirishi kwa kila mtu. Yogamāyā, yogamāyā inafunika," Kwa hivyo utamwonaje Mungu? Huu ni ujinga unaendelea, Kuwa "Unaweza kunionyesha Mungu? Umewai kumwona Mungu?" Mungu amekuwa kama kitu cha kuchezea. Huyu hapa Mungu. Yeye ni Mungu ameshuka duniani." (BG 7.15) Na māṁ duṣkṛtino mūḍhāḥ prapadyante narādhamāḥ Ni wenye dhambi, mtwana, wajinga, binaadm mwenye kiwango cha chini zaidi. Wanauliza hivyo. "Unaweza kunionyesha Mungu?" Umefuzu nini kumwona Mungu? Hili ndio la kufuzu. Iyo ni nini? Tac chraddadhānā munayaḥ. Mtu kwanza lazima awe mwaminifu. Mwaminifu. Śraddadhānāḥ. Kwa kweli, lazima awe na hamu ya kumwona Mungu. Sio hivi hivi ati "Unaweza kunionyesha Mungu?" Kiinimacho, ni kama Mungu ni kiinimacho La. Lazima awe mwaminifu sana: "Ndiyo, kama kuna Mungu... Tumeona, tumepashwa kumhusu Mungu. Kwa hivyo lazima nione."

Kuna hadithi kwenye muungano huu. Ina mafunzo mengi sana; Jribu kuskia. Msomaji mmoja mtaalam alikuwa akisoma kuhusu Bhāgavata, na alikuwa akieleza kuwa Krishna, amepambwa na majohari yote, Anatumwa kulinda ng'ombe msituni. Kulikuwa na mwizi kwenye huo mkutano. Kwa hivyo akafikiria kuwa "Mbona nisiende Vṛndāvana nimwibe kijana huyu? Yuko msituni na majohari mengi. Naeza kwenda nimshike na nichukue johari zote." Hiyo ndio ilikuwa niya yake. Kwa hivyo alikuwa na ujasiri kuwa, "Lazima nimpate kijana huyo. Na siku moja ntakuwa tajri. Majohari mengi. Sio" Kwa hivyo alienda, na fuzo lake ni kuwa. "Lazima nimwone Krishna, Lazima nimwone Krishna." Wasi wasi huo, hamu hiyo, ilimwezesha kumwona Krishna. Alimwona Krishna kma alivyo ambiwa na msomaji wa Bhāgavata Alafu akaona, "Oh, oh, wewe ni kijana mzuri sana, Krishna." Kwa hivyo alianza kumisfu. Alidhani kuwa "Nikimsifu, ntachukua johari zote." Kwa hivyo alipopendekeza lengo lake, "Kwa hivyo naweza kuchua mapambo haya? Wewe ni tajiri sana." "La, la, la. Wewe... Mamangu atakasirika. Siwezi..." Krishna kama mtoto. Kwa hivyo alikuwa na hamu zaidi na zaidi kwa Krishna. Alafu... Kwa kushirikiana na Krishna , alikuwa tayari amesafishwa. Na hatimaye, Krishna akasema, "Sawa basi, chukua." Alafu akawa mfuasi, mara moja. Kwa sababu kutokana na kushirikiana na Krishna...

Kwa hivyo, kwa njia moja au nyingine, lazima tushikamane na Krishna. Kwa njia moja au nyigine. Halafu tutasafishwa.