SW/Prabhupada 0012 - The Source of Knowledge Should Be By Hearing

Revision as of 05:14, 12 July 2019 by Vanibot (talk | contribs) (Vanibot #0023: VideoLocalizer - changed YouTube player to show hard-coded subtitles version)
(diff) ← Older revision | Latest revision (diff) | Newer revision → (diff)


Lecture on BG 16.7 -- Hawaii, February 3, 1975

Kila mmoja wetu, ana makosa fulani. Tunajivunia kwa kuwa tuna macho: "Unaweza kunionyesha?" Macho yako yana cheti ipi ya wewe kuona? Hafikirii hivyo, kuwa "Sina cheti lolote; lakini bado nataka kuona." Macho haya, oh, yanategemea masharti mengi sana. Saizi kuna stima, unaweza kuona. Pindi taa inapozima, huwezi kuona, Kwa hivyo macho yana maana gani? Huwezi kuona kile kinaendelea nyuma ya ukuta huu. Kwa hivyo usiamini fahamu zako kuwa kiini cha maarifa. La.

Kiini cha maarifa kinafaa kusikia. Hiyo inaitwa śruti. Kwa hivyo jina la Vedas ni śruti. Śruti-pramāṇa, śruti-pramāṇa. Kama vile mtoto au kijana anataka kujua babake ni nani. Kwa hivyo ushahidi uko wapi? Ushahidi ni śruti, kusikia kutoka kwa mama. Mama anasema, "Yeye ni babako." Kwa hivyo, haoni jinsi mtu huyo alikuja kuwa babake. Kwa sababu kabla ya mwili wake kuundwa, baba alikuwepo, angeonaje? Kwa hiyo kwa kuona, huwezi kusema babako ni nani. Lazima usikize kutoka kwa anayejua. Mama ndio anajua. śruti-pramāṇa: ushahidi ni kusikiza, sio kwa kuona. Kuona... macho ambayo hayaja kamilika... Kuna vikwazo vingi. Vile vile, kwa kutazama, huwezi kujua ukweli. Kutazama ni kubaatisha. Daktari Chura. DaktarI. Chura anabaatisha ukubwa wa bahari ya Atlantic. Yuko ndani ya kisima, kisima cha futi tatu, na rafiki yake anamwambia, "Oh, nimeona maji mengi." "Hiyo maji ni nini?" Bahari ya Atlantic "Ni kubwa kiasi gani?" Kubwa, Kubwa sana." Kwa hivyo Daktari Chura anafikiria, "Lbda futi nne. Kisima hichi ni futi tatu. Labda inaweza kuwa futi nne. Sawa sawa, futi tano. Sema kweli futi kum.i" Hivi, kwa kubaatisha, Daktari Chura ataelewaje Bahari Atlanta au Pacific? Je unaweza kukadiri upana na urefu wa Bahari Atlanta na Pacific kwa kubaatisha? Kwa hivyo kwa kubaatisha huwezi kupata. Kwa miaka mengi wanabaatisha kuhusu ulimwengu huu, nambari ya nyota zilizoko, Kitu fulani kina upana na urefu upi, kitu fulani kiko wapi... Hakuna anayejua hata kuhusu ulimwengu huu, na tutasemaji kuhusu dunia ya kiroho? Hii ni zaidi, mbali zaidi.

Paras tasmāt tu bhāvo 'nyo 'vyakto 'vyaktāt sanātanaḥ (BG 8.20). Utapata kwa Bhagavad-gītā. Kuna ulimwengu mwingine. Ulimwengu huu, kile unachoona, mbingu, kuba la duara, kuwa, juu ya hiyo tena kuna matabaka ya vipengele vitano. Hii ndio kifiniko. Kama vile nazi. Kuna kifiniko kigumu na ndani ya kifiniko hicho kuna maji. Vile vile ndani ya kifiniko hichi... Na nje ya kifiniko hicho kuna matabaka matano, ambayo yameshindana mara elfu moja kwa ukubwa; mtabaka wa maji, mtabaka wa hewa, mtabaka wa moto. Kwa hivyo nilazima upite matabaka hii. Alafu utafikia dunia ya kiroho. Malimwengu haya yote, isiyoweza kuhesabika, koṭi. Yasya prabhā prabhavato jagad-aṇḍa-koṭi (Bs. 5.40) Jagad-aṇḍa inamanisha ulimwengu. Koṭi, mamilioni yaliyo funganishwa pamoja, hiyo ndio dunia hii. Na baada ya dunia hii, kuna dunia ya kiroho, mbingu nyingine. Hiyo pia ni mbingu. Inaitwa paravyoma. Kwa hivyo kwa kutumia fahamu zako huwezi kudikiri hata kilicho kwenye jua au mwezi, Sayari hii, kwenye ulimwengu huu. Utaelewaje kuhusu dunia ya kiroho kwa kubaatisha? Huu ni ujinga.

Kwa hivyo śāstra (maandiko) inasema acintyāḥ khalu ye bhāvā na tāṁs tarkeṇa yojayet. Acintya, amabayo imepita fikra, zaidi ya fahamu zetu, haifai mtu ajaribu kuipinga au kuielewa kwa kubaatisha. Huu ni ujinga. Haiwezekani. Kwa hivyo tunapaswa kuenda kwa guru. Tad-vijñānārthaṁ sa gurum evābhigacchet, samit-pāṇiḥ śrotriyaṁ brahma-niṣṭham (MU 1.2.12). Hii ndio njia.