SW/Prabhupada 1060 - Mpaka mtu atakapo pokea hii Bhagavad-gita kwa moyo mtiifu



660219-20 - Lecture BG Introduction - New York

Sarvam etad ṛtaṁ manye (BG 10.14). "Naichukuwa, naamini kuwa yote uliyosema, ni kweli. Na nafsi yako ya Uungu, ni ngumu sana kuelewa kwa hivyo huwezi kutambulika hata na malaika. Huwezi kutambulika hata na malaika." Ina maana kuwa Mungu mkuu hawezi kutambulika hata na viumbe ambao wanamaarifa mengi kuliko binaadam, ni vipi binaadam anaweza kumwelewa Śrī Kṛishna bila kuwa mja wake?

Kwa hivyo Bhagavad-gītā inapaswa kupokewa na moyo wa mja wa Bwana Krishna. Mtu asidhani ati yeye yuko kwenye kiwango sawa na Śrī Kṛṣṇa, au mtu asidhani kuwa Krishna ni mtu wa kawaida, au labda ni mojawapo ya wakuu tu Hapana. Bwana Krishna ndio Mungu mkuu kwa hivyo kinadharia, kupitia matamshi yaliyoko kwenye Bhagavad-gītā au matamshi ya Arjuna, mtu ambae anajaribu kuelewa Bhagavad-gītā, anapaswa kumkubali Śrī Kṛṣhna kama Mungu mkuu, alafu, kwa hiyo moyo mtiifu... Mpaka mtu apokee Bhagavad-gītā hii, kwa moyo mtiifu na umakinifu wa kusikiza kama sivyo, itakuwa vigumu sana kuilewa kwa sababu ni siri kbwa sana.

Kwa hivyo katika Bhagavad-gītā... lazima tufanye utafiti kuhusu maana yake. Sababu ya Bhagavad-gītā ni kuokowa watu kutoka kwa ujinga wa maisha hii Kila mtu anashida kwa njia nyingi, kama Arjuna pia alikuwa na shida ya kupambana kwenye vita vya Kurukshetra. Na pindi alipojisalimisha kwa Śrī Kṛṣṇa, Bhagavad-gītā ilinenwa. Vivyo hivyo, sio Arjuna pekee ilhali kila mmoja wetu kawaida huwa na wasi wasi kwasababu ya maisha yetu hapa duniani Asad-grahāt. Yaani... Uhai wetu uko katika mazingira ya kutokuwa na uhai Walakini, huhai tunayo Maisha yetu ni ya uzima wa milele lakini kwa njia moja au nyingine tuko katika msimamo wa asat. Asat inamaanisha, ukosefu wa uhai Kati.

Ya binaadam wengi, nani kwa ukweli anajiuliza kwamba yeye nani, Mbona amewekwa katika hii hali uso stadi ya kuteseka... Mpaka mtu atakapofikia mahali ambapo atajiuliza, "Mbona nateseka? Sitaki haya mateso. Nimejaribu kutafuata majibu ya haya mateso, lakini nimeshindwa." Ila mtu atakuwa katika hali hii, hawezi semekana kuwa amekamilika kibinaadam. Ubinaadam, ni kuwa maswali kama haya yamezuka kwenye akili ya mtu. Haya maswali yanaitwa, brahma-jijñāsā, katika Brahma-sutra. Athāto brahma jijñāsā. Na shughli zote za binaadam hazina maana iwapo hakutakuwa na maswali haya katika akili ya mtu. Kwa hivyo mtu ambaye amezua maswali haya kwenye yake, Yani, "Mimi ni nani, mbona nateseka? Natoka wapi au nitaenda wapi baada ya kifo,? Pindi maswali haya yamezua kwenye bongo la mtu aliye na akili timamu, wakati huo basi, amehitimu kuwa mwanafunzi ambaye ataelewa Bhagavad-gita. Na ni lazma aweśraddhāvān. Śraddhāvān. Lazma awe na heshma, mpendano wa heshma kwa Mungu mukuu Mtu kama huyo, mfano bora in Arjuna.