SW/Prabhupada 1062 - Tuna tabia ya kutawala dunia

Revision as of 05:16, 12 July 2019 by Vanibot (talk | contribs) (Vanibot #0023: VideoLocalizer - changed YouTube player to show hard-coded subtitles version)
(diff) ← Older revision | Latest revision (diff) | Newer revision → (diff)


660219-20 - Lecture BG Introduction - New York

Kwa hivyo tunakosea. Tunaona vitu vya ajabu vikifanyika duniani, tunapaswa kujua kuwa nyuma ya udhiirisho huu wa ajabu, kuna mtawala hakuna linaloweza kudhirika bila kutawaliwa. itakuwa ni utoto tusipozingatia kuhusu mtawala. Kama vile gari nzuri, iliyo na spidi nzuri, na iliyo na uhandisi mzuri, inapokimbia kwenye barabara mtoto mdogo atafikiria, "Je hii gari inkimbia vipi" bila kusaidiwa na farasi au msukumo wowote? lakini mtu mwenye akili timamu au mtu mzima, anajua kuwa licha ya uhandisi huo wote kwenye gari hiyo bila kuwa na dereva, haiwezi kwenda. Uhandisi huo wa gari au katika kiwanda cha stima.. Sasa wakati huu ni wakati ambapo watu wanatumia mashine, lakini tunapaswa kujua kuwa chanzo cha mashine hiyo, chanzo cha machine hiyo hiyo kufanya kazi zake za kiajabu, ni dereva. Kwa hivyo Mungu mkuu ndio ndereve, adhyakṣa. Yeye ndio mkuu ambaye ndie chanzo cha kufanyika kwa kila kitu. Sasa hawa jīva, au viumbe, wamekubaliwa na Bwana kwenye hii Bhagavad-gītā, kama tutakavyo jua katika sura zijazo, kuwa hao ni kifurushi na sehemu ya Mungu mkuu. Mamaivāṁśo jīva-bhūtaḥ (BG 15.7). Aṁśa inamaanisha, kifurushi. Sasa kama vile chembe cha dhahabu, tone la maji ya bahari pia ni ya chumvi vile vile, sisi viumbe, kuwa furushi la mtawala mkuu, īśvara, Bhagavān, au Bwana Śrī Kṛṣṇa, tuna tabia sawa na Mungu mkuu, katika kiwango kidogo. kwa sababu sisi ni īśvara wadogo, tunajaribu kutawala pia tuna jaribu kutawala dunia tu. Siku hizi tunajaribu kutawala nafasi tunajaribu kuelesha masayari bandia. kwa hiyvo hii tabia ya kutawala au kuumba ipo kwa sababu tuna hiyo tabia ya kutawala kwa kiwango kidogo. Lakini tunapaswa kujua kuwa tabia hiyo haitoshi. Tuna tabia ya kutawala dunia, bali sisi sio watawala wakuu. Kwa hivyo hiyo imeelezwa kwenye Bhagavad-gītā.

Alafu dunia ni nini? Dunia pia aimeelezwa. Dunia imelezwa kwenye Bhagavad-gītā kuwa duni, prakṛti duni. na imeelezwa kuwa viumbe ni prakṛti. bora. Prakṛti inamaanisha, inayo tawaliwa, ambayo iko chini ya... maana halisi ya Prakṛti ni jike au mwanamke. Kama vile bwana anatawala vitendo vya bibi yake, vivyo hivyo, prakṛt iko chini ya utawala. Mungu mkuu yu mtawala, na hii prakṛti, viumbe pamoja na dunia, wanatawaliwa na Mkuu. Kwa hityo kulingana na Bhagavad-gītā, ingawa viumbe ni sehemu ya Mungu, wanachukuliwa kuwa prakṛti. Imetajwa wazi katika Sura ya Saba ya Bhagavad-gītā, apareyam itas tu viddhi aparā (BG 7.5). hii dunia ni aparā iyam. Itas tu, kando na hii kuna aina nyongine ya prakṛti. Na hiyo prakṛti ni gani? Jīva-bhūta, hawa...

Kwa hivyo hii prakṛti imepagawa na tabia tatu: hali njema, hali ya hamu na hali ya ujinga Na juu ya hali hizi tatu, kuna muda wa uliyo milele. na mchanganyiko wa hizi hali za dunia, chini ya utawala huu wa muda uliyo milele, kuna vitendo. Vitendo ambayo vinaitwa karma. Vitendo hivi vina fanyinyika tangu enzi na enzi na tuna teseka au kufurahia matunda ya vitendo vyetu.