SW/Prabhupada 0003 - Man Is Also Woman

From Vanipedia
Jump to: navigation, search
Go-previous.png Previous Page - Video 0002
Next Page - Video 0004 Go-next.png

Man Is Also Woman - Prabhupāda 0003


Lecture on SB 6.1.64-65 -- Vrndavana, September 1, 1975

tām eva toṣayām āsa
pitṛyeṇārthena yāvatā
grāmyair manoramaiḥ kāmaiḥ
prasīdeta yathā tathā
(SB 6.1.64)

Kwa hivyo baada ya kumwona mwanamke huyo, alikuwa akitafakari wakati wote, masaa ishirini na nne, kuhusu swala hilo, ukware. Kāmais tais tair hṛta-jñānāḥ (BG 7.20). Mtu anapokuwa na ukware, anapoteza maarifa yake. Dunia nzima inasukumwa na ukware huu. Dunia hii. Na kwa vili mimi ni mkware, we pia ni mkware; kila mmoja wetu, pindi tamaa zangu hazijatimizwa, tamaa zako hazzijatimizwa, basi nakuwa adui yako, nawe unakuwa adui yangu. Siwezi kuona unafanya maendeleo mazuri Huwezi kuona nafanya maendeleo mazuri. Dunia hii, wivu, tamaa, kāma, krodha, lobha, moha, mātsarya. Huu ndio msingi wa dunia hii.

Kwa hivyo akakuwa... Ni kuwa alikuwa akijifunza kuwa brāhmaṇa, śamo, dama, lakini maedeleo yake yakawa na makosa kwa sababu ya kushikamana na mwanamke. Kwa hivyo kulingana na ustaarabu wa Vedasi, mwanamke amekubaliwa kuwa kizuizi cha maendeleo ya kiroho. ustaarabu wote ni vile kuepuka... Mwanamke... Usifikiri kuwa mwanamke ni mwanamke tu. Mume pia ni mke. Usidhani kuwa mwanamke amelaaniwa; na mwanamume haja laaniwa. Mke inamaanisha mwenye kutoa faida na mume inamaanisha mfaidi. Kwa hivyo hii hisia hii imehukumiwa. Nikimuangalia mwanamke kama chombo cha kunifaidisha, mimi ni mume. Na mwanake akimwona mwanamme kama chombo cha kujifaidisha, ye pia ni mume. Mwanamke inamaanisha mwenye kutoa faida na mwanamume ni mfaidi. Kwa hivyo mtu yeyote mwenye hisia za kufaidi anachukuliwa kuwa mwanamme Kwa hivyo hapa jinsia zote mbili zimekusudiwa ku... Kila mmoja anapanga, Ntafaidi vipi? Kwa hiyo yeye ni puruṣa bandia. Ila kwa kweli, sisi sote ni prakṛti, jīva, aitha mke au mume. Hii ni nguo tu.