SW/Prabhupada 0013 - Twenty-four Hours Engagement



Lecture on BG 2.49-51 -- New York, April 5, 1966

Yogaḥ karmasu kauśalam. Kauśalam inamaanisha ujanja wa kiwango cha juu. Kama vile watu wawili wanafanya kazi. Mmoja ni mtaalam zaidi ilhali mwingine hana utaalam. Machine zote zina kasoro. Yule asiye na utaalam, atajaribu mchana na usiku, vile atakavyo irekebisha, lakini mtaalam akija, mara moja anaona kulipo na shida, na anaunganisha waya moja, huku na kule, na mashini inaanza kufanya. Hrzum, hrzum, hrzum, hrzum, hrzum, hrzum. Unaona? Kama vile wakati mwingine tunapata shida na kinasa sauti chetu, na Bwana. Carl au mtu mwingine anakuja kuirekebisha. Kwa hivyo kila kitu kina hitaji ujizi. Kwa hivyo karma inamaanisha kazi. Lazima tufanye kazi. Bila ya kufanya kazi hata miili yetu na roho zetu pia haziwezi kufanya kazi yao. Ni udanganyifu mkubwa kuwa, yule aliye... kwenye njia ya kutaka kujitambua kiroho hafai kufanya kazi. La, anafaa kufanya kazi zaidi. Watu ambao hawafuati njia hii ya kutaka kujitambua kiroho, wanaweza kushughulika kwa kazi masaa manane pekee, lakini walio kuwa kwenye njia hii ya kiroho, oh, wanashughulika masaa ishirini na nne, masaa ishirini na nne. Hiyo ndio tofauti. Na tofauti hiyo ni... Untapata kuwa duniani, kwenye mtazamo wa kimwili, ukifanya kazi kwa masaa manane pekee, usikia uchovu. Lakini kwa sabau ya kazi za kiroho. ukifanaya kazi zaidi ya masaa ishirini na nne... Kwa bahati mbaya, hatuna zaidi ya masaa ishirini na nne. Bado, hautachoka. Nawaambieni. Huu ni ushuuda wangu. Huu ni ushuhuda wangu. Na niko hapa, nafanya kazi ya kusoma au kuadika, Kusoma au kuandika, masaa ishirini na nne. Nikisikia njaa tu, nakula chafula. Na nikisikia usingizi tu, naeda kulala. la sivyo wakati wote, sichoki. Unaweza kummuliza Bwana. Paul kama sifanyi hivi. Kwa hivyo nafurahia kufanya hayo. Sichoki. Vile vile, mtu atakapo pata ufahamu wa kiroho, hata sikia... Bali, atalazimishwa kulala, kulala, Oh usingizi umekuja tu kunisumbua. Unaona? Anataka kupunguza masaa ya kulala. Alafu... sasa, tunaomba vande rūpa-sanātanau raghu-yugau śrī-jīva-gopālakau. Hawa Gosvāmī sita, walihimizwa na Bwana Caitanya kueleza sayansi hii. Wameandika vitabu vingi kuihusu. Unaona? Kwa hivyo utashangazwa kuwa walikuwa wakilala lisali moja na nusu pekee kila siku, sio zaidi ya hiyo. Kuwa saa zingine pia walikesha usiku na mchana.