Please join, like or share our Vanipedia Facebook Group
Go to Vaniquotes | Go to Vanisource | Go to Vanimedia


Vanipedia - the essence of Vedic knowledge

SW/Prabhupada 1063 - Tuepushe kutokana na matendo pamoja na matokeo ya matendo yetu yote

From Vanipedia


Give us Relief from the Actions and Reactions of all Activities - Prabhupāda 1063


660219-20 - Lecture BG Introduction - New York

Kama vile maisha ya sasa pia, tuna furahikia matunda ya matendo yetu. Tuseme mimi ni mwana biashara na kutumia akili, nimefanya bidii sana na nimepokea pesa nyingi sana. Wakati huo mimi ndio mwenye kufaidi Vile vile, tuseme nilianzisha biashara yangu na pesa nyingi sana, lakini nikashidwa kufaulu. Nikapoteza pesa nyingi sana. Sasa mimi ndio nateseka. Kwa hivyo, kataika kila jambo kwa maisha yetu, tunafaidi matokeo ya vitendo vyetu. Hii inaitwa karma.

Vitu hivi, īśvara, jīva, prakṛti, au Mungu mkuu, au kiumbe, dunia muda wa milele na vitendo vyetu tofauti, Vitu hivi vinaelezwa kwenye Bhagavad-gītā. Kati ya hizi tano, Bwana, Viumbe, dunia na muda, hivi vitu vinne vinaishi milele udhirisho wa prakṛti ingawa ni ya muda mfupi sio haina uongo. Wanafalsafa wanasema kuwa huu udhiirisho wa ulimwengu una uongo, lakini kulingana na falsafa ya Bhagavad-gītā au kulingana na falsafa ya wanavaishnava, hawakubaliani na udhiirisho wa ulimwengu kuwa na uongo. Wanakubali kuwa udhiirisho ni wakweli, ilhali ni wa muda mfupi tu. Ni kama vile wingu linachukua nafasi kwenye mbingu kisha msimu wa mvua unaaza, na baada ya msimu huo wa mvua kunakuwepo na mimea mingi, kwenye viwanja vyote. Tunaweza kuona Na pindi msimu wa mvua unapoisha, wingu hilo lina potea. Pole pole, mimea hii inakauka alafu tena ardhi inakauka. Vivyo hivyo, huu udhiirisho wa dunia infanyika kwa masaa fulani. Tutaelewa kwenye kurasa za Bhagavad-gītā. Bhūtvā bhūtvā pralīyate (BG 8.19). Huu udhiirisho unakuwa kwa masaa fulani na tena inapotea. Hio ndio kazi ya prakṛti. Lakini inatendeka milele, kwa hivyo prakṛti inaishi milele. Haina uongo. Kwa sababu Bwana ameikubali, mama prakṛti, "prakṛti. yangu." Apareyam itas tu viddhi me prakṛtiṁ parām (BG 7.5). Bhinnā prakṛti, bhinnā prakṛti, aparā prakṛti. Hii dunia ni nguvu tofauti za Mwenyezi Mungu, na viumbe vyote pia ni nguvu za Mwenyezi Mungu, ilhali ni nguvu tofauti pia. Wana uhusiano wa milele. Kwa hivyo, kiumbe, asili, asili ya dunia na muda, wote wanaishi milele. Lakini vitu hivyo vingine, karma, haiishi milele. Athari za vitendo vinaweza kuwa vya kale sana. Tunateseka au kufurahikia matokeo ya vitendo vyetu tangu enzi za kale, Lakini bado, tunaweza kubadilisha matokeo ya vitendo vyetu. Hii itategemea ukamilifu wa maarifa yetu. Tuna husika katika vitendo mbali mbali bila shaka, lakini hatujua in aina gani ya kazi tutatwaa ambayo ita tuepushe kutokana na matendo pamoja na matokeo ya matendo yetu. Hiyo imeelezwa kwa Bhagavad-gita pia.

Sasa, cheo cha Isvara ni fahamu iliyo kuu. Cheo cha Isvara au Mungu Mkuu, ni fahamu iliyo kuu. Na Majīva, au viumbe, hao kuwa furushi la Mungu Mkuu, pia anaufahamu. Kiumbe pia ana ufahamu. Imeelezwa kuwa kiumbe ni prakṛti, nguvu, na asili ya dunia pia ni prakṛti, lakini kati ya hizo mbili, prakṛti moja, majīva, wana ufahamau. prakṛti hiyo nyingine haina ufahamu. Hiyo ndio tofauti. Kwa hivyo, jīva prakṛti anaitwa bora kwa sababu majīva wana ufahamu sawiya na Bwana. Bwana ndiye fahamu iliyo kuu. Mtu hafai kudai kuwa jīva, kiumbe pia ndiye fahamu iliyo kuu. Hapana. Kiumbe hawezi kuwa na fahamu kuu wakati wowote kwenye ukamilifu wake. Huu mtazamo unapotosha. Ni mtazamo wa kupotosha. Ingawa ana ufahamu. Iyo tu. Lakini hana ufahamu ulio kuu.