SW/Prabhupada 0005 - Prabhupada's Life In 3 Minutes



Interview -- September 24, 1968, Seattle

Mhoji: Unaweza niambia kitu kuhusu historia yako? Yaani, mahali ulisomea, na vile ulikuja kuwa mwanafunzi wa Kṛṣṇa.

Prabhupāda: nilizaliwa na nikasomea Calcutta. Calcutta ndio nyumbani. nilizaliwa mwaka 1896,na nilikuwa mtoto-kipenzi cha babangu. hivyo kusoma kwangu kulichelewa kidogo. na bado, nilisoma katika shule ya upili,shule ya upili kwa miaka nane. shule ya msingi miaka nne ,shule ya upili miaka nane, na chuo, miaka nne. harafu nikajiunga na harakati ya Gandhi, harakati ya kitaifa. lakini kwa nafasi nzuri nilikutana na Guru Maharaja wangu, mwaka 19922. na tangu hapo ,nilivutiwa katika njia hii. na hatua kwa hatua nikaachana na maisha na shughuli za kifamilia. nilioa mwaka 1918 wakati huo nilikua mwanafunzi katika chuo mwaka wa tatu. Na hivyo nikapata watoto wangu. nilikuwa nafanya biashara. halafu nikastaafu kutoka maisha ya kifamilia mwaka 1954. miaka nne nilikuwa peke yangu, bila familia. halafu nikachukua ukawaida wa kasisi mwaka 1959. halafu nikajipeana katika uandishi wa vitabu. Uchapisho wangu wa kwanza ulitoka mwaka wa 1962, na wakati huo kulikuwa na vitabu tatu, halafu nikaanza katika nchi yenu mwaka 1965 nilifika hapa mwezi Septemba ,1965. tangu hapo,nijaribu kuhubiri huyu ufahamu wa Kṛṣṇa katika America Canada , na nchi za Europa. na hatua kwa hatua vituo vinaendelea. Wanafunzi pia wanaongezeka. hebu nione kile kitakachofanyika.

Mhoji; Ni kwa namna gani ulikuja kuwa mwanafunzi? nini ulikuwa,ama nini ulikuwa unafuata kabla ukuwe mwanafunzi?

Prabhupāda: kanuni sawa kama nilivyo kwambia, imani. Rafiki yangu mmoja, alinivuta kwa nguvu hadi kwa mwalimu wangu wa kiroho. na vile niliongea na mwalimu wangu wa kiroho , nilishawishika. na tangu hapo mmea ukaanza.