Please join, like or share our Vanipedia Facebook Group
Go to Vaniquotes | Go to Vanisource | Go to Vanimedia


Vanipedia - the essence of Vedic knowledge

SW/Prabhupada 0006 - Everyone is God - Fool's Paradise

From Vanipedia


Everyone Is God - Fool's Paradise - Prabhupāda 0006


Lecture on SB 1.15.49 -- Los Angeles, December 26, 1973

kila mtu anajivunia,kuwa "Najua. Najua kila kitu. kwa hivyo hakuna haja ya kwenda kwa guru." Hii ndio njia ya kwenda kwa guru, mwalimu mkuu wa kiroho. Salimu, kuwa "najua takataka nyingi sisizonamaana. Sasa kwa fadhili nifunze. Hii inaitwa kujiwasilisha. Kama vile Arjuna alisema, śiṣyas te 'haṁ śādhi māṁ prapannam [Bg. 2.7]. wakati kulikuwa na mabishano katikati ya Arjuna na Kṛṣṇa, na pale jambo halikusuluhishwa , wakati ule Arjuna alijiwasilisha kwa Kṛṣṇa, "Mpenzi Kṛṣṇa, sasa tunaongea kama marafiki. Hakuna kuongea tena kirafiki. nimekukubali kama mwalimu wangu mkuu wa kiroho. tafadhali nifunze kuhusu jukumu langu." hio ndio Bhagavad-gītā.

hivyo mtu lazima ajifunze. Tad-vijñānārthaṁ sa gurum eva abhigacchet [MU 1.2.12]. hii ndio amri ya maandiko ya Veda,kwamba nini thamani ya maisha? vile inavyobadilika? Vile tunavyopita kutoka mwili mmoja hadi mwingine? mimi ni nini? mimi ni hii mwili ama zaidi, kitu ingine? Hizi vitu lazima ziulizwe. hii ni maisha ya binadamu. Athāto brahma jijñāsā Kuuliza huku lazima kufanywe. kwa hivyo katika kali yuga, bila maarifa, bila kuuliza, bila mwalimu, bila kitabu chochote, kila mtu ni mungu. hii inaendelea, paradiso ya mjinga. kwa hivyo hii haitasaidia. hapa ,kuhusu Vidura...pia yeye...

viduro 'pi parityajya
prabhāse deham ātmanaḥ
kṛṣṇāveśena tac-cittaḥ
pitṛbhiḥ sva-kṣayaṁ yayau
(SB 1.15.49)

ali... nilikuwa naongea kuhusu Vidura. Vidura alikuwa Yamarāja. kwa hivyo mtu mtakatifu akaletwa mbele ya Yamarāja ndio aadhibiwe, hivyo wakati yule mtu mtakatifu aliuliza Yamarāja, kwamba "mimi ni..sikumbuki kuwa nimefanya dhambi yoyote maishani yangu. mbona nimeletwa hapa kuhukumiwa?" Hivyo Yamarāja akasema "Wewe hukumbuki. kuwa katika utotoni wako ulipitisha sindano moto katika njia ya haja kubwa ya mchwa akakufa. kwa hivyo lazima uadhibiwe." Ona tu. Katika utotoni, kwa ujinga, kwa sababu alifanya dhambi lazima angeadhibiwa. na kwa hiari yetu, tunaenda kinyume na kanuni ya kidini "usiue" tumefungua vyumba vingi vya kichinjio, huku tukupeana maelezo ya kijinga kwamba wanyama hawana roho. Ona mchezo tu. na hii inaendelea. Na tunataka kuwa na amani.