SW/Prabhupada 0010 - Don't Try To Imitate Krishna



Lecture on SB 7.9.9 -- Mayapur, February 16, 1976

Krishna... Bibi zake kumi na sita elfu, walikuwaje mabibi zake? Unajuwa hiyo hadithi kuwa, warembo kumi na sita elfu, mabinti wa wafalme walitekwa nyara na pepo. Jina la pepo huyo lilikuwa? Bhaumāsura, hapana? Ndio. Kwa hivyo walimwomba Krishna "Tunateseka, tumetekwa nyara na jinga hili. Tafadhali tuokowe." Kwa hivyo Krishna alikuja kuwakombowa, na Bhaumāsura akawawa na wasichna wote wakakombolewa. Lakini baada ya kukombolewawalikuwa bado wamesimama hapo. Kwa hivyo Krishna akawaambia, "Sasa mnaweza kuenda nyumbani kwa baba zenu." Wakasema kuwa "Tumetekwa nyara, na hatuwezi kuolewa." Kule India sheria hiyo bado iko. Ikiwa msichana mmoja mdogo ametoka nyumbani kwa siku moja au mbili, hakuna atakaye muoa. Hakuna atakaye muoa. Anachukuliwa kama aliyeharibika. Hii ni sheria ya India bado. Kwa hivyo walikuwa wametekwa nyara kwa siku nyingi sana au miaka mingi sana, kwa hivyo wakamwomba Krishan kuwa "Hatuta kubaliwa hata na baba yetu, wala hakuna atakaye kubali kutuoa." Na Krishna kaelewa kuwa "Hali yao ni ngumu sana. Ilhali wamekombolewa, hawewezi kwenda popote." Alafu Krishna...Yeye ni mkarimu, bhakta-vatsala. Akauliza, "Mwatakaje?" Wakasema kuwa "Tukubali. Kama sivyo hatuna njia yoyote ya kuishi." Krishna mara moja: "Ndiyo, Kujeni." Huyo ni Krishna. Na sio ati bibi zake kumi na sita elfu walikuwa wamejaa katika kambi moja. Mara moja alijenga ikulu elfu kumi na sita. Kwa sababu aliyemkubali kama bibi, nilazima akae kama bibi yake, kama malkia, sio ati "Kwa sababu hawana njia nyingine yoyote, wamekimbilia ulinzi wangu. Niwaweke tu." Hapana. Kwa heshima zote kama malkia, malkia wa Krishna. Na tena akafikiria kuwa "Mabibi elfu kumi na sita... Kwa hivyo nikiwa peke yangu, basi bibi zagu hawawezi kukutana nami. Kila mmoja lazima angoje siku elfu kumi na sita kumwona bwana yao. Sivyo." Alijipanua mara elfukumi na sita Krishna. Huyo ni Krishna. Wajinga, wanamshtaki Krishna kuwa mkware. Sio kama wewe. Huwezi kumtunza hata mwanamke mmoja, lakini alitunza mabibi kumi na sita elfu kwenye ikulu elfu kumi na sita na kwa upanuzi kumi na sita elfu ya umbo lake. Kila mmoja alifurahi. Huyo ndiye Krishna. Lazima tumwelewe Krishna. Usijaribu kumwigiza Krishna. Kwanza kabisa jaribu mwelewa Krishna.