SW/Prabhupada 0011 - One Can Worship Krishna Within The Mind

From Vanipedia
Jump to: navigation, search
Go-previous.png Previous Page - Video 0010
Next Page - Video 0012 Go-next.png

One Can Worship Kṛṣṇa Within The Mind - Prabhupāda 0011


Lecture on BG 4.28 -- Bombay, April 17, 1974

Kwenye Bhakti-rasāmṛta- sindhu, kuna hadithi... Sio hadithi. Ukweli. Imeelezwa kuwa brāhmaṇa mmoja alikuwa mfuasi mkubwa sana - alikuwa anataka kutoa huduma nzuri mno, kwenye hekalu. Lakini hakuwa na pesa yoyote. Lakini siku moja alikuwa amekaa kwenye darasa la Bhāgavata na akasikia kuwa Krishna anaweza kuabudiwa akilini pia. Kwa hivyo akachukuwa fursa hii kwa sababu alikuwa akifikiria kwa muda mrefu vile ambavyo ata mwabudu Krishna vizuri kabisa, lakini hakuwa na pesa.

Kwa hivyo aliposikia kuwa mtu anaweza kumwabudu Krishna akilini, baada ya kuoga kwenye Mto Godāvarī, alikuwa amekaa chini ya mti na kwenye akili yake alikuwa akijenga siṁhāsana, nzuri sana, iliyo pambwa na vito na kuweka sanamu ya Mungu katika kiti cha enzi, alikuwa akimwogesha na maji ya Ganges, Yamunā, Godāvarī, Narmadā, Kāverī. alafu alikuwa akimvisha nguo vizuri sana, alafu kumwabudu kwa kutumia maua na taji za maua.

Alafu alikuwa akipika vizuri sana, alikuwa akipika paramānna, wali mtamu. Kwa hivyo alitaka kujuwa, ikiwa ilikuwa moto sana. Kwa sababu paramānna inaliwa wakati imepoa. Paramānna hailiwi ikiwa moto. Kwa hivyo aliweka kidole chake kwenye paramānna na kidole chake kikachomeka. Kisha mtafakara wake ukakatizwa wa sababu hakukuwa na kitu. Kwenye akili yake tu alikuwa akifanya kila kitu. Lakini akaona kuwa kidole chake kimechomeka. Kwa hivyo alishtuka.

Kwa njia hii, Nārāyaṇa kutoka Vaikuṇṭha, alikuwa akitabasamu. Lakṣmījī akauliza, "Mbona watabasamu?" "Mfuasi wangu mmoja ananiabudu hivi. Tuma watu wangu wamlete Vaikuṇṭha mara moja."

Kwa hivyo bhakti-yoga ni nzuri sana kuwa, hata kama huna uwezo wa kumwabudu Mungu kwa mali nyingi, unaweza kumwabudu akilini. Hiyo pia inawezekana.