SW/Prabhupada 0017 - Two energies are working in this material world: the spiritual energy and the material energy



Lecture on Sri Isopanisad, Mantra 1 -- Los Angeles, May 2, 1970

Kwa hivyo nishati mbili zinafanya kazi katika hii dunia: nishati ya kiroho na ya dunia. Nishati ya dunia inamaanisha vipengele vinane vya dunia. Bhūmir āpo 'nalo vāyuḥ: (BG 7.4) ardhi, maji, moto, hewa, mbingu, ubongo, akili na nafsi. Haya yote ni ya dunia. Na vile vile laini, laini, laini. laini na pato, pato, pato. Kama vile maji ni laini kuliko ardhi, alafu moto ni laini kuliko maji, alafu hewa ni laini kuliko moto alafu mbingu au ombwe ni laini kuliko hewa. Vile vile akili ni laini kuliko ombwe, au bongo ni laini kuliko ombwe. Bongo... nimepeana, mfano huu mara nyingi: Maelfu ya maili unayoweza kufika kwa mwendo wa sekunde moja Kwa hivyo, inavyokuwa laini zaidi ndivyo inavyo kuwa na nguvu zaidi Vile vile, mwishowe ukifikia kwenye sehemu ya kiroho, laini, ambapo kila kitu inatokea, oh, hiyo inanguvu sana. Hiyo nishati ya kiroho. Imepeanwa kwenye Bhagavad-gītā. Iyo nishati ya kiroho ni ipi? Hiyo nishati ya kiroho ni kiumbe. Apareyam itas tu viddhi me prakṛtiṁ parā (BG 7.5). Krishna anasema, "Nishati hii ya dunia. Baada ya hii kuna nyingine, nishati ya kiroho." Apareyam. Aparā inamanisha duni. Apareyam. "Vipengele hivi vyote vilivyo tajwa vya kidunia ni duni. Na baada ya haya, kuna nishati bora zaidi, Mpedwa wangu Arjuna." Iyo ni gani? Jīva-bhūta mahā-bāho: "Viumbe hawa." Hao pia ni nishati. Sisi viumbe, pia ni nishati, nishati iliyo bora. Bora vipi? Kwa sababu yayedaṁ dhāryate jagat (BG 7.5). Nishati bora inatwala nishati duni. Rasilmali za dunia havina nguvu. Ndege kubwa, yeynye mashini nzuri, inapepea angani, imetengenezwa na rasilmali za dunia. Lakini mpaka kuwe na nishati ya kiroho, dereva, haiwezi kuwa na maana. Haiwezi kuwa na maana. Maelfu ya miaka mpaka sasa, ndege itasimama kituoni; haiwezi kupepea mpaka chembe kidogo cha nishati ya kiroho, yaani dereva akuje aiguse. Kwa hivyo kuna ugumu upi wa kumwelewa Mungu? Kitu wazi kabisa, kuwa ikiwa mashini hii kubwa... Kuna mashini nyingi kubwa kubwa, haziwezi kusogea bila mguso wa nishati ya kiroho, binaadam au kiumbe. Unawezaje kutarajia kuwa nishati hii ya dunia ifanye kazi kimiujiza au bila mwongozo? Utawezaje kuleta ubishi wako kwa njia hii? Hiyo haiwezekani. Kwa hivyo wenye akili duni, hawawezi kuelewa vile nishati hii ya dunia inaongozwa na Mwenyezi Mungu.