SW/Prabhupada 0026 - You Are First of all Transferred to the Universe Where Krishna is

From Vanipedia
Jump to: navigation, search
Go-previous.png Previous Page - Video 0025
Next Page - Video 0027 Go-next.png

You Are First of all Transferred to the Universe
Where Kṛṣṇa is - Prabhupāda 0026


Morning Walk -- October 5, 1975, Mauritius

Indian man: Swamijī, imesemekana vile tu si hufanya... Tunazaliwa kulingana na vitendo vyetu. Hivyo iwapo tumefanya kitu lazima tuzaliwe kulingana na sheria ya Mungu.

Prabhupāda: Lazima uzaliwe. Hio ni ukweli. huweziepuka. Lakini kulingana na na vitendo vyako lazima uzaliwe.

Indian man: Lakini basi... Hii inamaanisha kuwa utalipa kile uliandika. Ndio, eh? Hiyo unafikiria kuwa....

Prabhupāda: Tuseme wakati, hili shati litararuka, lazima ununue shati lingine. Sasa, Hilo shati uko nalo lazima ununue kulingana na bei yako. Kama uko na pesa nzuri, basi unapata shati nzuri. kama hauna pesa basi hutapata shati.

Indian man: Nilikuwa nataka kusema hivi, Swamijī, kuwa jehanamu pia imejengwa katika ulimwengu huu, kwa sababu unafikiria ni wapi tunawezalipa deni yetu aje? Dhambi, deni ya dhambi zetu. Unafikiria tutalipia wapi? Katika jehanamu, na sio..

Prabhupāda: Jehanamu ni mahali pa adhabu.

Indian man: Hivyo basi iko kwa hii dunia.

Prabhupāda: Mbona dunia?

Indian man: Katika sayari ya dunia, sio?

Prabhupāda: Hapana. haiwezi kuwa....

Indian man: Kwa sayari zozote?

Prabhupāda: ...mamilioni ya maili kwa umbali

Indian man: Lakini haijawekwa mahali...Jehanamu pekee imechapishwa mahali pamoja ama mahali pengine? Unadhani hivyo, Swamijī?

Prabhupāda: Ndio. Ndio. Kuna sayari tofauti.

Indian man: Kuna watu wengi wanaoteseka katika dunia hii .

Prabhupāda: Hivyo kwanza kabla ya yote wanafunzwa katika sayari ya jehanamu halafu wanakuja kuteseka katika hali hio ya maisha.

Indian man: wakati roho zetu zimetoka kwa kwa mwili, zinaenda jehanamu au...

Prabhupāda: Sayari ya jehanamu.

Indian man:..au baadaye wanazaliwa mara moja?

Prabhupāda: Ndio. Wale wenye dhambi, huwa hawazaliwi mara tu. Kwanza huwa wanafunzwa katika sayari ya jehanamu namna ya kuteseka ndio wazoee halafu wanazaliwa tena, ndio wateseke. Kama vile kupita mtihani wa I.A.S. Halafu ukawa msaidizi wa hakimu. Unasoma. Halafu ukawekwa kama hakimu. Hata kama umehitimu kurudi nyumbani, nyumbani kwa Mwenyezi Mungu, kwanza unahamishwa kwa ulimwengu ambako Kṛṣṇa ako, na hapo ndipo unazoea. Halafu unaenda Vṛndāvana halisi.

Indian man Hivyo, baada ya kifo chetu...

Prabhupāda; Mpango wote wa Mungu ni mkamilifu. Pūrṇam. Pūrṇam adaḥ pūrṇam idaṁ pūrṇāt pūrṇam.. (Īśopaniṣad, Invocation). Kile ambacho Mungu ameumba ni kikamilifu.