SW/Prabhupada 0027 - They do Not Know That There is Next Life

From Vanipedia
Jump to: navigation, search
Go-previous.png Previous Page - Video 0026
Next Page - Video 0028 Go-next.png

They do Not Know That There is Next Life -
Prabhupāda 0027


Lecture on CC Adi-lila 7.1 -- Atlanta, March 1, 1975

Hivyo (kusoma:) "Mtu aliyekatika hali ya mashaarti maishani ako katika hali ya unyonge. Lakini binadanu katika hii dunia, chini ya udanganyifu na nguvu ya dunia au ya nje, hudhani kwamba amelindwa na nchi yake kabisa, jamii, urafiki, na mapenzi, bila kujua kuwa katika wakati wa kifo hakuna hata mmoja wa hawa anaweza kumuokoa." Hii inaitwa udanganyikaji. Lakini haamini. Chini ya udanganyifu, haamini pia nini maana ya kuokoa. Kuokoa. Kuokoa inamaana ya kumuokoa mtu kutokana na marudio, ya kuzaliwa na kufa. Hio ndio kuokoa halisi. Lakini hawajui. (Kusoma:) "Sheria za maumbile ya dunia ziko na nguvu sana kwamba hakuna kilicho chetu. kinaweza kutuokoa kutokana na mikono ya kifo katili." Kila mtu anajua hivo. Na hio ndio shida yetu. Nani haogopi kifo? Kila mtu anaogopa kifo. kwa nini? Kwa sababu kila kiumbe, hikafai kufa. Ni kiumbe cha kuishi milele;kwa hivyo kuzaliwa,kufa ,uzee na ugonjwa hizi vitu ni zakumsumbua. Kwa sababu yeye ni wa milele, huwa hazaliwi, na jāyate, na yule ambaye hazaliwi, huwa hakufi pia, na mriyate kadācit. Hii ndio nafasi yetu halisi. Kwa hivyo tunaogopa kifo. Huo ndio mwelekeo wetu kimaumbile.

Hivyo kutuokoa kutokana na kifo..... Hio ndio biashara ya kwanza ya uanadamu. Tunafunza huu ufahamu wa Kṛṣṇa kwa lengo hili pekee. Hilo ndilo linafaa kuwa lengo la kila mtu. Hilo ndilo amri la maandiko. Wale ambao ni walezi... Serikali, baba, mwalimu, ni walezi wa watoto. Wanapasawa kujua , namna ya kulinda watoto kutokana na ya ulimwengu... Na mocayed yaḥ samupeta mṛtyum. Hivyo hii filosofia iko wapi, duniani popote? Hakuna filosofia kama hii. Hii ndio pekee, ufahamu wa Kṛṣṇa, inaoweka mbele filosofia hii, sio kimchezomchezo lakini imeidhinishwa na maandiko, maandiko ya Veda, mamlaka. Hivyo hiko ndilo ombi letu. Tunafungua vituo tofauti duniani kote kwa manufaa ya jamii kuwa hawajui lengo la maisha, hawajui kwamba kuna maisha ingine baada ya kifo. Hizi vitu hawajui. Kuna maisha ingine bila shaka, na unaweza tayarisha maisha yako ijayo. Unaweza enda kwenye mfumo wa sayari za juu kwa ajili ya starehe, starehe mali. Unaweza kaa hapa katika nafasi salama." Salama inamaana hii maisha ya dunia. Kama ilvyosemwa,

yānti deva-vratā devān
pitṟn yānti pitṛ-vratāḥ
bhūtāni yānti bhūtejyā
mad-yājino 'pi yānti mām
(BG 9.25)

Hivyo unawezajitayarisha kwa ajili ya maisha nzuri kwenye sayari za binguni, au katika jamii nzuri hapa duniani ama kwenda kwa sayari ambako vizuka na wengine wabaya wanadhibiti. Au unaweza enda kwa sayari aliyoko Kṛṣṇa. Kila kitu ni wazi kwako. Yānti bhūtejyā bhūtāni mad-yājino 'pi yānti mām. Rahisi lazima ujitayarishe. Kama vile katika maisha ya ujana unapata elimu- mtu fulani atakua mhandisi, mtu fulaini atukua mtu wa matibabu,mwingine atakua wakili na wataalamu wengine wengi- na wanajitayarisha kwa kusoma, kwa njia sawa, unawezajitayarisha kwa ajili ya maisha ijayo. Hii si ngumu kuelewa. Lakini hawaamini kuhusu maisha ijayo, hata ingawa ni kitu ya kawaida. Kweli kuna maisha ijayo kwa sababu Kṛṣṇa anasema na tunaezaelewa filosofia kwa akili kidogo kwamba kuna maisha ijayo. Kwa hivyo pendekezo letu ni kuwa "Iwapo lazima ujitayarishe kwa ajili ya maisha ijayo, basi kwanini usishughulike kujitayarisha kwa ajili ya kurudi nyumbani, nyumbani kwa Mwenyezi Mungu?" Hili ndilo pendekezo letu.