Please join, like or share our Vanipedia Facebook Group
Go to Vaniquotes | Go to Vanisource | Go to Vanimedia


Vanipedia - the essence of Vedic knowledge

SW/Prabhupada 1057 - Tuepushe kutokana na matendo pamoja na matokeo ya matendo yetu yote

From Vanipedia


Bhagavad-gita is Known also as Gitopanisad, the Essence of Vedic Knowledge - Prabhupāda 1057


660219-20 - Lecture BG Introduction - New York

Prabhupada:

oṁ ajñāna-timirāndhasya
jñānāñjana-śalākayā
cakṣur unmīlitaṁ yena
tasmai śrī-gurave namaḥ

(Natoa unyenyekevu wangu kwa mwalimu wangu wa kiroho kwa heshima ambae kwa kutumia tochi ya maarifa amefungua macho yangu iliokuwa imepofushwa na giza la ujinga)

śrī-caitanya-mano-'bhīṣṭaṁ
sthāpitaṁ yena bhū-tale
svayaṁ rūpaḥ kadā mahyaṁ
dadāti sva-padāntikam

(Ni lini Śrīla Rūpa Gosvāmī Prabhupāda, ambae ameanzisha katika hii dunia ya vifaa ujumbe wa kutimiza mapenzi ya Bwana Caitanya, atanipa makaazi chini ya miguu yake yenye maumbile ya jani la ua.)

vande 'haṁ śrī-guroḥ śrī-yuta-pada-kamalaṁ śrī-gurūn vaiṣṇavāṁś ca
śrī-rūpaṁ sāgrajātaṁ saha-gaṇa-raghunāthānvitaṁ taṁ sa-jīvam
sādvaitaṁ sāvadhūtaṁ parijana-sahitaṁ kṛṣṇa-caitanya-devaṁ
śrī-rādhā-kṛṣṇa-pādān saha-gaṇa-lalitā-śrī-viśākhānvitāṁś ca

(Natoa heshima kwa unyenyekevu wangu chini ya miguu ya mwalimu wangu wa kiroho na walimu wengine wote ambao wako katika njia hii ya huduma ya ibada. Natoa heshima kwa unyenyekevu wangu kwa Mavaishnava wote na kwa ma Goswami sita, kwa pamoja na Śrīla Rūpa Gosvāmī, Śrīla Sanātana Gosvāmī, Raghunātha dāsa Gosvāmī, Jīva Gosvāmī na washirika wao. Natoa heshima kwa unyenyekevu wangu kwa Śrī Advaita Ācārya Prabhu, Śrī Nityānanda Prabhu, Śrī Caitanya Mahāprabhu, na waja wote, wakiongozwa na Śrīvāsa Ṭhākura. Alafu natoa heshima kwa unyenyekevu wangu chini ya miguu ya Bwana Krishna, Śrīmatī Rādhārāṇī na magopi wote wakiongozwa na Lalitā na Viśākhā.)

he kṛṣṇa karuṇā-sindho
dīna-bandho jagat-pate
gopeśa gopikā-kānta
rādhā-kānta namo 'stu te

(O mpenzi wangu Kṛṣṇa, wewe ni bahari ya huruma, na rafiki ya wale walioko kwenye mashaka na ndio chanzo cha viumbe vyote. Wewe ni mwalimu wa kundi la walinzi wa ng'ombe na mpenzi wa magopi hasa Rādhārāṇī. Natoa heshima kwa unyenyekevu wangu kwako.)

tapta-kāñcana-gaurāṅgi
rādhe vṛndāvaneśvari
vṛṣabhānu-sute devi
praṇamāmi hari-priye

(Natoa heshima kwa unyenyekevu wangu kwa Rādhārāṇī, ambae rangi ya mwili wake ni kama dhahabu iliyoyeyushwa na ambae ni malkia wa Vṛndāvana. Wewe ni binti ya mfalme Vṛṣabhānu, na ni mpendwa zaidi wa Bwana Kṛṣṇa.)

vāñchā-kalpatarubhyaś ca
kṛpā-sindhubhya eva ca
patitānāṁ pāvanebhyo
vaiṣṇavebhyo namo namaḥ

(Natoa heshima kwa unyenyekevu wangu kwa ma Vaiṣṇava wote ambao ni waja wa Bwana. Wanaweza kutimiza hamu ya kila mtu, kama vile miti ya kutimiza hamu na wamejawa na huruma kwa watu wote walionguka.)

śrī-kṛṣṇa-caitanya
prabhu-nityānanda
śrī-advaita gadādhara
śrīvāsādi-gaura-bhakta-vṛnda

(Natoa heshima kwa unyenyekevu wangu kwa Śrī Kṛṣṇa Caitanya, Prabhu Nityānanda, Śrī Advaita, Gadādhara, Śrīvāsa na waja wote wa Bwana Caitanya.)

hare kṛṣṇa hare kṛṣṇa kṛṣṇa kṛṣṇa hare hare
hare rāma hare rāma rāma rāma hare hare

(Bwana wangu mpendwa na nguvu zako za kiroho, tafadhali nishirikishe katika huduma yako. Wakati huu nimeaibishwa nahuduma hii ya kidunia. Tafadhali nishirikishe na huduma yako.)

Mwanzo wa Gītopaniṣad na A.C. Bhaktivedanta Swami, mwandishi wa Śrīmad-Bhāgavatam, Easy Journey to Other Planets, mhariri wa Back to Godhead, na kadhalika.

Bhagavad-gītā inajulikana kwa majina mengine kama Gītopaniṣad, kiini cha maarifa ya Vedasi, moja wapo ya Upanishadi muhimu zaidi katika vitabu vya Vedasi. Hii Bhagavad-gītā, ina waandishi wengi katika lugha ya kimombo na umuhimu wa uandishi huu kwa kimombo inaweza kufafanuliwa kwa njia hii Moja... Mwanamke mmoja wa Kiamerika, Bi Charlotte Le Blanc aliniambia nipendekeza tolea la Bhagavad-gītā kwa kimombo ambayo angeweza kusoma. Kama kawaida Amerika kuna toleo nyingi za Bhagavad-gītā kwa kimombo lakini mpaka sasa nimeweza kuziona, sio Amerika peke yake bali India pia hakuna moja wapo ambayo inaweza semekana madhubuti kuwa na mamlaka. kwa sababu karibia kila moja yao imeelezea maoni ya watu binafsi kupitia maelezo ya Bhagavad-gītā bila kugusa roho ya Bhagavad-gītā kama ilivyo.

Roho ya Bhagavad-gītā, imetajwa katika Bhagavad-gītā yenyewe. Ni kama hivi. Ikiwa tunataka kumeza dawa fulani lazma tufuate maelezo ambayo yameelezwa katika lebo ya dawa hiyo. Hatuezi kumeza dawa, kulingana na maelezo yetu wenyewe au maelezo ya rafiki, ila tunaweza kumeza dawa kulingana na maelezo ambayo imepeanwa katika lebo ya chupa na ambayo imepeanwa na daktari. Vile vile, Bhagavad-gītā pia inafaa kuchukuliwa au kukubaliwa kama ilivyoelezwa moja kwa moja na msemaji Mwenyewe.