SW/Prabhupada 1058 - Msemaji wa Bhagavad-gita ni Bwana Krishna



660219-20 - Lecture BG Introduction - New York

Msemaji wa Bhagavad-gita ni Bwana Krishna. Anatajwa katika kila ukurasa wa Bhagavad-gītā, kama Mungu mkuu aliye na utu, Bhagavān. Bila shaka, "bhagavān" inatumika wakati mwengine tunapo ongea kuhusu mtu yeyote aliye na nguvu au malaika yeyote aliye na nguvu, lakini hapa bhagavān kwa hakika inamrejelea Śrī Kṛṣṇa, mtu mkubwa ajabu, wakati huo huo lazima tujue kuwa Bwana Śrī Kṛṣṇa, kama alivyo thibitishwa na walimu wote watangulizi... Śaṅkarācārya, Rāmānujācārya, Madhvācārya, Nimbārka Svāmī na Śrī Caitanya Mahāprabhu na wengine wengi. Kule India kulikuwa na wasomi na walimu wengi walio kubalika, yaani walio kubalika kumiliki maarifa ya Vedasi. Wote pamoja na Śaṅkarācārya, wamemkubali Śrī Kṛṣṇa kama Mungu mkuu. Bwana pia amejitambulisha mwenyewe kama Mungu mkuu katika kurasa za Bhagavad-gītā. Amekubalika kwenye Brahmā-saṁhitā na Purāṇa zote, sana sana kwenye Bhāgavata Purāṇa: kṛṣṇas tu bhagavān svayam (SB 1.3.28). Kwa hiyo tunapaswa kuchukulia Bhagavad-gītā kama ilivyonenwa na Mungu mkuu mwenyewe. katika ukurasa wa nne wa Bhagavad-gītā Bwana anasema:

imaṁ vivasvate yogaṁ
proktavān aham avyayam
vivasvān manave prāha
manur ikṣvākave 'bravīt
(BG 4.1)
evaṁ paramparā-prāptam
imaṁ rājarṣayo viduḥ
sa kāleneha mahatā
yogo naṣṭaḥ parantapa
(BG 4.2)
sa evāyaṁ mayā te 'dya
yogaḥ proktaḥ purātanaḥ
bhakto 'si me sakhā ceti
rahasyaṁ hy etad uttamam
(BG 4.3)

Bwana alimwambia Arjuna kuwa "Huu mfumo wa yoga ya Bhagavad-gītā, nilimnenea mfalme wa jua kwanza na mfalme wa jua akamweleza Manu. Manu akamwelezea Ikṣvāku, na kupitia hiyo njia ya mfululizo wa nidhamu, moja baada ya nyingine huu mfumo wa yoga inatujia, na katika mwendo wa wakati, huu mfumo umepotea sasa. Kwa hiyo, nakueleza kuhusu mfumo ule ule wa yoga kwa mara nyingine, ule ule mfumo wakitambo wa yoga ya Bhagavad-gītā, au Gītopaniṣad. Kwasababu wewe ni mja wangu na rafiki yangu pia, kwa hiyo kunauwezekano kuwa utaelewa."

Maelezo ni kuwa Bhagavad-gītā ni mkataba ambao umenenwa hasa kwa ajili ya waja wa Bwana. Kuna aina tatu ya waumini, kwa majina, jnani, yogi na bhakta. ama muimpasonalisti, mtafakari na mja. imesemwa wazi. Bwana anamwambia Arjuna kuwa "Nakueleza au nakufanya kuwa mwalimu wa kwanza katika mfululizo wa walimu katika maarifa hii. Kwa sababu nidhamu ya mfululizo wa kitambo umevunjwa, nataka kuanzisha mfululizo mwengine tena. katika mfululizo huo huo wa kimawazo, kama ilivyo kuja chini kutoka kwa mfalme wa jua kufikia wengine. Kwa hiyo, ichukue na uisambaze. au mfumo huu wa yoga ya Bhagavad-gītā ita sambazwa sasa kupitia kwako. chukua mamlaka ya kuelewa Bhagavad-gītā." inaelekezwa hapa kuwa Bhagavad-gītā imenenwa hasa kwa Arjuna, mja wa Bwana, mwanafunzi myoofu wa Krishna. na sio hiyo peke yake, ana uhusiano wa undani na Krishna kama rafiki. Kwa hiyo Bhagavad-gītā inaeleweka na mtu aliye na tabia sawa na Krishna. Ina maanisha kuwa lazima awe mja, lazima awe na uhusiano wa moja kwa moja na Bwana.