SW/Prabhupada 1068 - Kuna vitendo vya aiana tatu kulingana na Hali tatu za asili ya dunia

From Vanipedia
Jump to: navigation, search
Go-previous.png Previous Page - Video 1067
Next Page - Video 1069 Go-next.png

There are Three Kinds of Activities according to the Different Modes of Nature - Prabhupāda 1068


660219-20 - Lecture BG Introduction - New York

Kuna vitendo vya aiana tatu kulingana na Hali tatu za asili ya dunia Bwana akiwa pūrṇam kwa njia zote, kamwe hadhibitiwi na sheria za dunia hii. Kwa hivyo mtu anapaswa kuwa na hekima kujua kuwa hakuna mtu anaye miliki chochote ulimwenguni. Hiyo imeelezwa kwenye Bhagavad-gītā:

ahaṁ sarvasya prabhavo
mattaḥ sarvaṁ pravartate
iti matvā bhajante māṁ
budhā bhāva-samanvitāḥ
(BG 10.8)

Bwana ndiye muumba asili. Yeye ni muumba wa Brahmā, Ni muumba... Iyo pia imeelezwa. Yeye ni Muumba wa Brahmā. Kwenye sura ya Kumi na moja, Bwana ameitwa kwa majina prapitāmaha (BG 11.39) kwa sababu Brahmā ameitwa pitāmaha yaani babu, lakini Bwana ni muumba wa babu pia. Kwa hivyo mtu yoyote asiseme kuwa anamiliki chochote. Mtu anafaa ku kubali vitu ambavyo amepewa na Bwana kujimudu. Kuna njia nyingi amabazo tunaweza kutumia tulivyo pewa na Bwana Iyo pia imeelezwa kwenye Bhagavad-gītā. Mwanzoni Arjuna aliamua kutopigana vita. Iyo ilikuwa mtazamo wake. Alimwambia Bwana kuwa haikuwa na uwezekano wake kufurahia ufalme wa jamaa zake. Huo mtazamo ulikuwa wa dhana ya mwili. Kwa sababau alikuwa akifikiria kuwa mwili wake ulikuwa yeye, na jamaa zake wa kimwili, ndugu zake, wapwa, babake mkwe au babu yake walikuwa upanuzi wa mwili wake, na alikuwa akifikiria hizo ili kutosheleza matakwa yake ya kimwili. Na hayo yote yaliongewa na Bwana kubadilisha mtazamo wake. Na akakubali kutenda kulingana na matakwa ya Bwana. Na akasema, kariṣye vacanaṁ tava (BG 18.73)

Kwa hivyo katika hii dunia binadamu hawafai kugombana kama mapaka na maumbwa. wanafaa kuwa na akili ya kutosha kugundua umuhimu wa maisha ya mwanadamu. na kukataa kutenda kama mnyama wa kawaida. Binadamu anafaa kugundua lengo la maisha ya mwanadamu. Mwelekeo huu umepeanwa kwenye maadiko ya Vedasi na kiini hicho kimepenwa kwenye Bhagavad-gītā. Maandiko haya yameandikwa kwa ajili ya wanadamu sio mapaka na maumbwa. Paka na Umbwa wanaweza kuua wanyama wengine kama kitoweo chao. Kwa hiyo hawapati dhambi. Lakini binaadam akiua mnyama ili kutosheleza ulimi wake isioweza kudhibiti lazima awajibike kwa kuvunja sheria za dunia. Na kwenye Bhagavad-gītā imeelezwa wazi kuna vitendo vya aina tatu kulingana na hali za asili ya dunia: Vitendo vya hali ya uzuri, vitendo vya halitamaa, vitendo vya hali ya ujinga. Vile vile, kuna vyakula vya aina tatu pia: vyakula vya uzuri au njema, vyakula vya tamaa na vyakula vya ujinga. Yote yameelezwa wazi, na tukielewa mafunzo ya Bhagavad-gītā vizuri, maisha yetu yote itasafishwa na hatimaye tutafika mwisho wa safari yetu. Yad gatvā na nivartante tad dhāma paramaṁ mama (BG 15.6).

Ujumbe huo umepeanwa kwenye Bhagavad-gītā, kuwa baada ya anga hii ya kidunia, kuna anga nyingine ya kiroho, iitwayo anga ya sanātana. Kwenye anga iliyofunikwa, kila kitu kinakaa kwa muda mfupi tu. Inadhiirishwa kwa muda mfupi, kutupa matokeo fulani, kisha inanyauka na kupotea. Iyo ni sheria ya dunia hii. Kwa mfano mwili huu au tunda au kitu chochote ambacho kimeumbwa lazima kiangamie mwishowe. Kwa hivyo zaidi ya dunia hii ya muda mfupi kuna dunia nyingine ambabyo ujumbe upo, paras tasmāt tu bhāvaḥ anyaḥ (BG 8.20). kuna dunia nyingine iishiyo milele sanātana, iishiyo milele. Na imelezwa kuwa jīva ni sanātana. Mamaivāṁśo jīva-bhūtaḥ jīva-loke sanātanaḥ (BG 15.7). Sanātana, sanātana inamaanisha milele. Na sura ya kumi na moja imeeleza kuwa Bwana yu sanātana. Kwa hivyo tuna uhusiano wa undani kabisa na Bwana, na sote kwa jumla tuna tabia sawa... sanātana-dhama, na Mungu Mkuu aliye sanātana na viumbe waliyo sanātana, wako kwenye kiwango sasa kitabia. Kwa hivyo lengo la Bhagavad-gītā ni kuzindua cheo chetu kama sanātana inajulikana kama sanātana-dharma, au cheo cha kiumbe iishiyo milele. Wakati huu tunashiriki katika vitendo tofauti kwa muda mfupi. tunapo epukana na vitendo hivvi, sarva-dharmān parityajya (BG 18.66), Maisha takatifu ni wtunakubali vitendo ampendekezayo Mwenyezi Mungu