SW/Prabhupada 1069 - Dini inawasilisha dhana ya Imani, Imani inaweza kubadilika - lakini Sanatana haiwezi

From Vanipedia
Jump to: navigation, search
Go-previous.png Previous Page - Video 1068
Next Page - Video 1070 Go-next.png

Religion Conveys the Idea of Faith. Faith May Change - Sanatana-dharma Cannot - Prabhupāda 1069


660219-20 - Lecture BG Introduction - New York

Kwa hivyo kama ilivyo tajwa ya kwamba Mwenyezi Mungu yu sanātana, na makaazi yake takatifu, juu ya mbingu pia ni sanātana. na viumbe vyote pia ni sanātana. Kwa hivyo mahusiano ya Mwenyezi Mungu aliye sanātana na viumbe vyote walio sanātana, kwenye makaazi yake ambayo ni sanātana pia, hatimaye ndio lengo la maisha ya mwanadamu. Bwana yu mkarimu kwa viumbe vyote kwa sababu viumbe vyote wanasemekana kuwa wana wa Mwenyezi Mungu. Bwana anasema sarva-yoniṣu kaunteya sambhavanti mūrtayo yāḥ (BG 14.4). Viumbe vyote... Kuna viumbe vya aina tofauti kulingana na karma walizonazo, lakini Bwana anasema kuwa yeye ndiye baba ya viumbe vyote, na Bwana anashuka ili kukomboa viumbe vyote waliosahaulika kuwarejesha kwenye sanātana-dhāma, mbingu iliyo sanātana ili viumbe hao walio sanātana warejee kwenye cheo cha mahusianao yao na Bwana. Anakuja mweneyewe na maumbile yake tofauti. Ana watuma wajakazi wake wa undani kama wana au washiriki au walimu ili kurejesha roho zilizo potea.

N kwa hivyo sanātana-dharma sio aina yoyote ya dini. Nicheo halisi viumbe wote ambao wana uhusiano wa milele na Mwenyezi Mungu. Kufikia sasa sanātana-dharma inamaanisha cheo cha milele. Śrīpāda Rāmānujācārya amaeeleza neno sanātana kuwa kuwa kitu ambacho hakina mwanzo wala mwisho. Na tunapo ongea kuhusu sanātana-dharma hatufai kusahau maneno ya Śrīpāda Rāmānujācārya kuwa haina mwanza wala mwisho. Neno dini ni tofauti kidogo na sanātana-dharma. Dini inaangazia dhana ya imani. Imani inaweza kubadilika. Mtu anaweza kuwa na imani na mchakato fulani na anaweza kubadilisha imani yake na atwae imani nyingine. Walakini sanātana-dharma haiwezi kubadilika. Kama vile maji na unyevu. Unyevu haiwezi kubadilishwa kuto kuwa maji. Joto na moto. Joto haiwezi kubadilishwa kuto kuwa moto. Vile vile, cheo cha milele cha kiumbe inajulikana kama sanātana-dharma, haiwezi kubadilishwa. Haiwezi kubadilika. Lazima tujue cheo chake kiumbe. Tunapo ong'ea kuhusu sanātana-dharma tusisahau maneno ya Śrīpāda Rāmānujācārya kuwa haina mwanzo wala mwisho. Kitu ambacho hakina mwanzo wala mwisho sio lazima kiwe kitu ambacho hakizidi mipaka ya mafikira yetu. Tunapo ong'ea kuhusu sanātana-dharma, kuna watu wa dini zingine wanaweza kukosea na kufikiria kuwa ni dini fulani. Lakini tukizama kwenye swala hilo na tuzingatie mtazamo wa sayansi ya kisasa, tutaweza kuiona sanātana-dharma kuwa kitu cha watu wote duniani, yaani viumbe vyote ulimwenguni. Dini zisizokuwa sanātana zinaweza kuebuka kutoka kwa historia ya jamii ya wanadamu, lakini hakuwezi kuwa na historia ya sanātana-dharma kwa sababu sanātana-dharma inabaki kuebuka na historia ya viumbe. Kwenye maandiko kufikia sasa tunapata kuwa viumbe pia hazaliwi wala hawafi/ Imesemekana kwenye Bhagavad-gītā ya kuwa kiumbe, hazaliwi kamwe, hafi kamwe anaishi milile, hawezi kuangamizwa, na anazidi kuishi hata baada ya mwili wake kuanagmizwa.