SW/Prabhupada 1073 - Ikiwa hatuaacha hii tabia ya kutaka kumiliki dunia hii

From Vanipedia
Jump to: navigation, search
Go-previous.png Previous Page - Video 1072
Next Page - Video 1074 Go-next.png

So Long We Do Not Give Up this Propensity of Lording it Over the Material Nature - Prabhupāda 1073


660219-20 - Lecture BG Introduction - New York

Kwenye sura ya kumi na tano ya Bhagavad-gītā, picha kamili ya dunia hii imepeanwa inasemekana hapo kuwa

ūrdhva-mūlam adhaḥ-śākham
aśvatthaṁ prāhur avyayam
chandāṁsi yasya parṇāni
yas taṁ veda sa veda-vit
(BG 15.1)

Dunia hii imeelezwa kwenye sura ya kumi na tano ya Bhagavad-gītā Kama mtii iliyo na mizi yake juu, ūrdhva-mūlam. Je umewai kuona mti wowote ambao miziz yake iko juu? Tuna uzoefu wa kuona mti kama huu kwenye akisi. Tukisimama kanzo ya ziwa au mahali popote palipo na maji, tunaweza kuona kuwa mti kando ya ziwa imeakisiwa kwenye maji ikiwa na shina chini na mzizi ujiwa juu. Kwa hiyvo dunia hii dunia ni akisio la dunia ya kiroho. Kama vile akisio la mti kwenye ziwa inaonekana kuangalia chini. vile vile dunia hii inaitwa kivuli. Kivuli Kama vivulini hamna ukweli wowote, lakini kwa wakati huo huo kupitia kivuli tunaweza kufahamu kuwa kuna hali halisi. Mfano wa kivuli cha maji jangwani, inaonyesha kuwa jagwani hamna maji lakini, tunaweza kivuli cha maji. Vile vile dunia hii ni kivuli cha duniya ya kiroho, hakika hakuana furaha, hakuna maji. Lakini maji halisi au radhi halisi iko kwenye dunia ya kiroho. Bwana anasema kuwa ni lazima mtu afikie dunia hiyo ya kiroho kwa njia hii, nirmāna-mohā.

nirmāna-mohā jita-saṅga-doṣā
adhyātma-nityā vinivṛtta-kāmāḥ
dvandvair vimuktāḥ sukha-duḥkha-saṁjñair
gacchanty amūḍhāḥ padam avyayaṁ tat
(BG 15.5).

Kuwa padam avyaya, ufalme huo wa milele, unaweza kufkiwa na mtu ambaye ni nirmāna-mohā. Nirmāna-mohā inamanisha tunataka cheo. Tunataka vyeo kwa njia fulani ambazo ni bandia, Kwa mfano, mtu fulani anataka kuwa mdosi, mwengini anataka kuwa bwana mtu mwengine anataka kuwa rais, mwingine anataka kuwa tajiri au mwingine, mfalme. cheo hivi vyote, ikiwa bado tutashikamana na vyeo hivi... Kwa sababu vyeo hivi vyote ni vya kimwili. Bali sisi sio mwili huu. Hii ndiyo mtazamo wa kwanza wa maono ya kiroho. Kwa hivyo mtu asishikamane na vyeo. Na jita-saṅga-doṣā, saṅga-doṣā. Wakati huu tunashirikiana na hali tatu za dunia, na tutakapo kitenga kupitia huduma ya ibada ya Bwana... Ikiwa hatuja vutiwa na huduma ya ibada ya Bwana, hatuwezi kujitenga na hali tatu za kidunia. Kwa hivyo Bwana anasema, vinivṛtta-kāmāḥ, vyeo hivi au mshikamano wetu ni kwa ajili ya tamaa. Tunataka kumiliki dunia. Ikiwa hatuta wacha hii tabia ya kutaka kutawala dunia, mpaka tutakapo fikia hapo basi hakuta kuwa na uwezekano wetu wa kufikia ufalme wa Mwenyezi, yaani sanātana-dhāma. Dvandvair vimuktāḥ sukha-duḥkha-saṁjñair gacchanty amūḍhāḥ, amūḍhāḥ padam avyayaṁ tat (BG 15.5). Ufalme wa milele, ambayo hai angamizwi kamwe kama hii dunia, inaweza kukaribiwa na amūḍhāḥ. Amūḍhāḥ inamaanisha timamau, mtu ambaye hasumbuliwi na mvutio wa faida ya kiongo. Na ambaye amekita katika huduma kuu ya Bwana, ndiye anayefaa kufikia ufalme wa milele. Na ufalme wa milele hauhitaji jua, wala mwezi wala stima. Iyo ni kiojo cha mada ya kufikia ufalme wa milele.