SW/Prabhupada 1072 - Kuacha dunia hii na kupata maisha yetu daima kwenye ufalame wa milele

From Vanipedia
Jump to: navigation, search
Go-previous.png Previous Page - Video 1071
Next Page - Video 1073 Go-next.png

Leaving this Material World and get our Eternal Life in the Eternal Kingdom - Prabhupāda 1072


660219-20 - Lecture BG Introduction - New York

Bwana kwa neema zake anajitokeza na umbo lake la Śyāmasundara-rūpa. Kwa bahati mbaya watu wenye mafikira duni wanamzomea. Avajānanti māṁ mūḍhā (BG 9.11). Kwa sababu Bwana anakuja kama moja wetu na kucheza nasi kama binaadam, kwa hivyo hatupaswi kufikiria kuwa Bwana ni mmoja wetu. Kwa nguvu zake, anajitokeza na umbo lake kamili mbele yetu na kuonyesha visa vyake, mfumo wa makazi yake. Kwa hivyo makaazi ya Bwana ina sayari nyingi isiyo weza kuhesabika Kama vile kuna sayari nyingi ambazo zina elea kwenye nuru za jua vile vile, kwenye brahma-jyotir, itokayo kwa makaazi ya Mwenyezi Mungu, Kṛṣṇaloka, Goloka, ānanda-cinmaya-rasa-pratibhāvitābhis (BS 5.37), sayari zote hizo ni za kiroho. Zi ānanda-cinmaya; sio sayari za ki dunia Kwa hivyo Bwana anasema

na tad bhāsayate sūryo
na śaśāṅko na pāvakaḥ
yad gatvā na nivartante
tad dhāma paramaṁ mama
(BG 15.6)

Mtu yeyote anayeweza kufikia hiyo sayari ya kiroho hata hitajika kurudi kwa hii dunia kamwe. Ikiwa tuka katika dunia hii, tutasemaje kuhusu kufikia sayari ya mwezi... Mwezi ndio sayari iliyo karibu, lakini hatu tukifikia sayari ya juu zaidi, ambayo inaitwa Brahmaloka, pia tutapata taabu zile zile za maisha, yaani taabu ya kuzaliwa, kuzeeka na magonjwa. Hakuna sayari yoyote kwenye ulimwengu huu ambayo ina epukana na kanuni nne za maisha ya dunia. Kwa hivyo Bwana anasema kwenye Bhagavad-gītā, ya kuwa,ābrahma-bhuvanāl lokāḥ punar āvartino 'rjuna (BG 8.16). Viumbe wanasafiri kutoka kwa sayari moja kwenda nyingine. Sio ati tunaweza kufikia sayari zingine kwa njia zetu za sputnik. Kuna mbinu za kufikia sayari zingine, ikiwa mtu anataka. Yānti deva-vratā devān pitṟn yānti pitṛ-vratāḥ (BG 9.25). Ikiwa mtu anataka kwenda kwa sayari nyingine, kwa mfano mwezi, hatufai kutumia mbinu ya sputnik. Bhagavad-gītā inatueleza kuwa, yānti deva-vratā devān. Sayari ya mwezi au jua au nyingine yoyote iliyozidi Bhūloka, inaitwa Svargaloka. Svargaloka. Bhūloka, Bhuvarloka, Svargaloka. Kuna viwango tofauti vya sayari. Zinajulikana kama Devaloka. Bhagavad-gītā inapeana mfumo rahisi sana ya kufikia sayari zilizo juu, yaani Devaloka. Yānti deva-vratā devān. Yānti deva-vratā devān. Deva-vratā, tukijifunza njia ya kuabudu kijiungu fulani, kisha tufikia sayari hio pia. Tunaweza kufikia sayari ya jua, mwezi au sayari zilizoko mbinguni, Walakini Bhagavad-gītā haitushauri kwenda kwenye sayari hizi za kidunia, kwa sababu tukifikia Brahmaloka, sayari iliyo juu zaidi, ambayo imehesabiwa na wana sayansi wa kisasa kuwa tutachukua miaka elfu arubaini kufikia sayari iliyo juu zaidi ikiwa tuna safiri kwa mwendo wa sputniki. Haiwezekani mtu kuishi miaka elfu arubaini kufikia sayari ya juu zaidi kwenye ulimwengu huu. Lakini ikiwa mtu ameishi maisha yake akimwabudu kijiungu fulani, anaweza kufikia sayari hiyo, kama ilivyo semekana kwa Bhagavad-gītā kuwa: yānti deva-vratā devān pitṟn yānti pitṛ-vratāḥ (BG 9.25). Vile vile kuna Pitṛloka. Anayetaka kufikia sayari kuu yaani Kṛṣṇaloka. Kwenye mbingu ya kiroho kuna sayari zisizo weza kuhesabika, yaani sayari zilizo daima, amabazo haziangamizwi kamwe. Lakini kati ya sayari zote za kiroho kuna sayari moja, halisi inayoitwa Goloka Vṛndāvana. Taarifa hizi ziko kwenye Bhagavad-gītā na tumepewa nafasi ya kutoka kwenye hii dunia ili tupate uzima wetu wa milele kwenye ufalme wa milele.