SW/Prabhupada 1076 - Wakati wa kifo, tunaweza kubaki hapa au kuhamishwa kwenye Dunia ya Kiroho

From Vanipedia
Jump to: navigation, search
Go-previous.png Previous Page - Video 1075
Next Page - Video 1077 Go-next.png

At the Time of Death We Can Remain Here, or Transfer Into the Spiritual World - Prabhupāda 1076


660219-20 - Lecture BG Introduction - New York

Haya ni mabhāva tofauti. Sasa, mazingira hii ya dunia pia ni mojawapo ya mabhāva, kama tulivyo eleza, ya kwamba mazingira haya ya dunia pia ni maonyesho ya nguvu zake Mwenyezi Mungu. Viṣṇu Purāṇa imepeana muhtasari wa nguvu zote za Mwenyezi Mungu kwa jumla.

viṣṇu-śaktiḥ parā proktā
kṣetra-jñākhyā tathā par
avidyā-karma-saṁjñānyā
tṛtīyā śaktir iṣyate
(CC Madhya 6.154)

Nguvu hizi zote, za... Parāsya śaktir vividhaiva śrūyate (CC Madhya 13.65, maelezo). Mwenyezi Mungu ana nguvu mbali mbali, ambazo haziwezi kuhesabika wala kufikirika. Lakini watakatifu wakuu walio na maarifa yaani roho zilizo nusuliwa, wamwetafiti na hatimaye kuhitimisha kwa kugawanya nguvu zote kwenye vipengele vitatu. Ya kwanza... Nguvu zote ni viṣṇu-śakti. Nguvu hizo zote ni nishati tofauti za Bwana Viṣṇu. Nishati hiyo ni parā, kuu. Na kṣetra-jñākhyā tathā parā, na viumbe vyote ni kṣetra-jña, hao pia ni wanatoka kwenye kundi la nishati ikiyo kuu, kama ilivyo thibitishwa kwenye Bhagavad-gītā. Tushaeleza. Na nishati hiyo nyingineyo, nishati ya dunia hii ni tṛtīyā karma-saṁjñānyā (CC Madhya 6.154). Nishati hiyo iko katika hali ya ujinga. Hiyo ndiyo nishati ya dunia hii. Kwa hivyo, wakati wa kifo, tunaweza kubaki kwenye nishati hii ya dunia, au tunaweza kusafirishwa kwenye dinia ya kiroho. Hiyo ndiyo kigrzo. Kwa hivyo Bhagavad-gītā inasema,

yaṁ yaṁ vāpi smaran bhāvaṁ
tyajaty ante kalevaram
taṁ tam evaiti kaunteya
sadā tad-bhāva-bhāvitaḥ
(BG 8.6)

Kama vile tumezoea kuwaza, aitha kuhusu nishati ya dunia hii au ya dunia ile ya kiroho, tunawezaje kubadilisha mawazo hayo? Mawazo ya nishati ya dunia hii itabadilishwaje, kuwa mawazo ya nishati ya kiroho? Kwa hivyo, maadiko ya Vedasi yamepeana njia ya kuwaza kuhusu nishati za kiroho. Kama vile kuna maadiko mengi ya kuwaza katika njia ya kidunia magazeti, majarida, riwaya, tetesi na mengineyo mengi. Zimejawa na maadishi. Na mawazo yetu yamefyonzwa kwenye maadishi haya. Vile vile, ikiwa tunataka kugeuza mafikira yetu yawe katika mazingara ya kiroho, basi sharti tugeuze kiwango cha usomi wetu katika maadiko ya Vedasi. Watakatifu walio na maarifa waliandika vitabu vingi vya Vedasi, kama vile Purāṇas. Purāṇas sio hadithi. Ni rekodi za historia. Kwenye Caitanya-caritāmṛta kuna mstari ambayo inasema hivi, Anādi-bahirmukha jīva kṛṣṇa bhuli' gela ataeva kṛṣṇa veda-purāṇa kailā (CC Madhya 20.117). Yakuwa viumbe hawa wasahaulifu, wamesahau uhusiano wao na Mwenyezi Mungu, na mezama katika mawazo ya vitendo vya kidunia. Na ili kugeuza uwezo wao wa kufikiria katika hali ya kiroho, Kṛṣṇa-dvaipāyana Vyāsa, amaeunda vitabu vindi ya Vedasi. Maadiko ya Vedasi inamaanisha kuwa aligawa Vedasi kwenye vipengele vinne. Alafu akayaeleza kupitia kwa Purāṇas. Alafu kwa yule asojiweza kama vile strī, śūdra, vaiśya, aliandika Mahābhārata. Na kwenye Mahābhārata alianzisha Bhagavad-gītā hii. Alafu akatoa muhstari wote wa maadiko ya Vedasi kwenye Vedānta-sūtra. Amabayo ni ya mwongozo wa baadaye, yeye mwenyewe aliandika Śrīmad-Bhāgavatam.