SW/Prabhupada 1077 - Bwana yu mkamilifu, Hakuna tofauti kati ya jina lake na yeye mwenyewe

From Vanipedia
Jump to: navigation, search
Go-previous.png Previous Page - Video 1076
Next Page - Video 1078 Go-next.png

The Lord Being Absolute, There is No Difference Between His Name and Himself - Prabhupāda 1077


660219-20 - Lecture BG Introduction - New York

Śrīmad-Bhāgavatam inaitwa bhāṣyo 'yaṁ brahma-sūtrāṇām. Ni maandiko halisi ya Vedānta-sūtra. Kwa hivyo maadikao haya yote, tukibadilisha mawazo yetu tad-bhāva-bhāvitaḥ, sadā. Sadā tad-bhāva-bhāvitaḥ (BG 8.6). Mtu ambaye anahusika wakati wote... Kama vile mtu dunia wakati wote anahusika katika usomi wa maandiko ya kidunia, kama vile magazeti, majarida na tetesi, riwaya nakadhalika, falsafa nyingi za kisayansi, vitu hivi vyote vyeneye viwango tofauti ki fikra. Vile vile, tukibalisha kiwango cha usomi wetu na kusoma vitabu hivi vya Vedasi, kama vilovyopeanwa kwa ukarimu na Vyāsadeva, basi itawezekana tumkumbuke Mwenyezi Mungu wakati wa kifo chetu. Hii ndio njia pekee iliyopendekezwa na Bwana mwenyewe. Sio kupendekezwa, ni hakika. Nāsty atra saṁśayaḥ (BG 8.5). Bila shaka. Hakuna mashaka kuhusu swala hilo. Tasmāt, Bwana amependekeza, kwa hivyo tasmāt sarveṣu kāleṣu mām anusmara yudhya ca (BG 8.7). Anamshauri Arjuna kuwa mām anusmara yudhya ca. Hasemi, "We nifikirie tu na uwache kazi zako unazofanya wakati huu." Hapana. Hiyo haijashauriwa. Bwana hashauri kitu kisicho wezekana kamwe. Dunia hii, ilikutunza mwili huu, mtu lazima afanye kazi. Kazi imegawanywa kwenye vipengele vinne vya jamii. brāhmaṇa, kṣatriya, vaiśya, śūdra. Walio na maarifa katika jamii wanafanya kazi kwa njia tofauti, Wasimamizi katika jamii pia wanafanya kazi kwa njia tofauti. Jamii ya wanabiashara, wenye kuto mazao katika jamii pia wanafanya kazi kwa njia tofauti, na wafanyi kazi pia wanafanya kazi kwa njia tofauti. Katika jamii ya wanadamu, aitha kama mfanyi kazi au mwanabiashara au wanasiasa, wasimamizi, au wenye kiwango cha juu cha maarifa katika masomo, utafiti wa kisayansi, kila mtu anashiriki katika kazi fulani, na mtu nilazima afanye kazi, apambane maishani.

Kwa hiyo Bwana anashauri kuwa, "Sio lazima uwache kazi yako, lakini kwa wakati huo huo unaweza kukumbuka. Mām anusmara (BG 8.7). Iyo itakufanya, itakusaidia kunikumbuka wakati wa kifo chako. Kama hautajifunza kunikumbuka kila wakati, pamoja na mpambano wako maishani, basi hauiwezekani." Haiwezekani. Jambo hilo pia limeshauriwa na Bwana Caitanya, kīrtanīyaḥ sadā hariḥ (CC Adi 17.31). Kīrtanīyaḥ sadā. Mtu anafaa kujifunza kukariri jina la Bwana wakati wote. Jina la Bwana na Bwana mwenyewe haina tofauti. Kwa hivyo mafunzo ya Bwana Krishna kwa Arjuna hapa ni kuwa mām anusmara (BG 8.7), "We nikumbuke tu," na funzo la Bwana Caitanya kuwa "Kariri jina la Krishna wakati wote." Hapa Krishna anasema "Nikumbuke wakati wote," au umkumbuuke Krishna, na Bwana Caitanya anasema, "Kariri jina la Krishana wakati wote." Kwa hivyo hakuna tofauti kwa sababu Krishna na jina lake hawatofautiani. Kwenye hadhi kuu hakuna tofauti kati ya kitu kimoja na kingine. Iyo ndiyo hadhi kuu. Kwa sababu Bwana yu kwenye hadhi kuu, hakuna tofauti kati ya jina lake na Yeye mwenyewe. Kwa hivyo ni lazima tujifunze kwa njia hiyo. tasmāt sarveṣu kāleṣu (BG 8.7) Wakati wote, masaa ishirini na nne, ni lazima tujenge vitendo vyetu maishani kwa njia ambayo tunaweza kukumbuka, masaa ishirini na nne. Inawezekanaje? Ndiyo, inawezekana. Inawezekana. Mfano umepeanwa na maācārya kwa swala hili. Na mfano huo ni upi? Inasemekana kuwa mwanamke ambaye ameshikamana na mwanaume mwingine hata kama ana bwana, ikiwa bado ameshikamana na mwanamume mwingine. Mshikamano huu inakuwa na nguvu sana. Hii inaitwa parakīya-rasa. Aitha kwa mwanamume au mwanamke. Ikiwa mwanamumu amaeshikana na mwanamke mwingine isipokuwa bibi yake, au mwanamke amaeshikamana ma mume mwingine isipokuwa bwanake, mshikamano huo unakuwa na nguvu sana, Mshikamano huo una nguvu sana. Kwa hivyo maācārya wamepeana mfano huu kuwa mwanamke mwenye tabia mbaya ambaye anashikamana na bwana wa wenyewe, wakati huo huo anafikiria, anamwonyesha bwanake kuwa anahusika sana kwenye maswala ya familia ili bwanake asishuku tabia yake. Kwa hivyo wakati wote anafikiria vile atakutana na mpenzi wake usiku, hata baada ya kufanya kazi hizi za nyumba vizuri sana, vile vile mtu lazima amkumbuke Bwana mkuu, Śrī Kṛṣṇa, wakati wote hata baada ya kufanya kazi zake zakidunia vizuri sana. Hiyo inawezekana. Inahitaji mapenzi yenye nguvu.