SW/Prabhupada 1080 - Muhtasari kwenye Bhagavad-gita - Mungu mmoja ni Krishna. Krishna sio Mungu wa kidini

From Vanipedia
Jump to: navigation, search
Go-previous.png Previous Page - Video 1079
Next Page - Video 0001 Go-next.png

Muhtasari kwenye Bhagavad-gita - Mungu mmoja ni Krishna. Krishna sio Mungu wa kidini - Prabhupāda 1080


660219-20 - Lecture BG Introduction - New York

Bwana anasema kwa nguvu sana mwishoni mwa Bhagavad-gītā ahaṁ tvāṁ sarva-pāpebhyo mokṣayiṣyāmi mā śucaḥ (BG 18.66). Bwana amechukua muajibiko. Atakaye jisajili kwa Bwaba, anachukua muajibiko wa kumwokowa, Kumwokowa kutoka kwa matokeo ya dhambi zake.

mala-nirmocanaṁ puṁsāṁ
jala-snānaṁ dine dine
sakṛd gītāmṛta-snānam
saṁsāra-mala-nāśanam
(Gītā-māhātmya 3)

Mtu hujisafisha kilasiku kwa kuoga majini, lakini anaye oga mara moja kwenye maji takatifu ya Ganges ya Bhagavad-gītā, maisha yake chafu inaangamizwa.

gītā su-gītā kartavyā
kim anyaiḥ śāstra-vistaraiḥ
yā svayaṁ padmanābhasya
mukha-padmād viniḥsṛtā
(Gītā-māhātmya 4)

Kwa sababu Bhagavad-gītā imeongewa na Mwenyezi Mungu, watu wanafaa ku... Watu wanaweza wasi some vitabu vyote vya Vedasi. ila akiskiza mara kwa mara kwa maakini na mara kwa mara kusikiza na kusoma Bhagavad-gītā, gītā su-gītā kartavyā... Na mtu anafaa kufuata njia hii kwa njia zote. Gītā su-gītā kartavyā kim anyaiḥ śāstra-vistaraiḥ. Kwa sababu nyakati hizi, watu wanaaibishwa na vitu vingi, amabapo ni vigumu kuchepua masikio yake kwenye maadiko yote ya Vedasi. Kitabu hiki kimoja kita wachepua kwa sabau ndio kiini cha maadiko vote ya Vedasi, na sana sana imeongelewa na Mwenyezi Mungu.

bhāratāmṛta-sarvasvaṁ
viṣṇu-vaktrād viniḥsṛtam
gītā-gaṅgodakaṁ pītvā
punar janma na vidyate
(Gītā-māhātmya 5)

Kama ilivyo semekana kuwa atakaye kunywa maji ya Ganges, yeye pia anaokolewa, je tutasemaje kuhusu Bhagavad-gītā? Bhagavad-gītā ndio nta kwenye Mahābhārata yote, na imeongelewa na Viṣṇu. Bwana Krishna ndiye Viṣṇu asili. Viṣṇu-vaktrād viniḥsṛtam. Inatoka kwa mdomo wa Mwenyezi Mungu. Na gaṅgodakaṁ, Ganges inasemekana kutoka kwa miguu ya Bwana, na Bhagavad-gītā imetoka kwa mdomo wa Bwana. Kama kawaida hakuna tofauti kati ya mdomo na miguu ya Mwenyezi Mungu. Bado, tunaweza kutafiti kuwa Bhagavad-gītā ni muhimu zaidi kishinda maji ya Ganges.

sarvopaniṣado gāvo
dogdhā gopāla-nandana
pārtho vatsaḥ su-dhīr bhoktā
dugdhaṁ gītāmṛtaṁ mahat
(Gītā-māhātmya 6)

Kama... Hii Gītopaniṣad ni kama tu ng'ombe, na Bwana anajulikana ka mlinzi wa ng'ombe na alikuwa akimkamua huyu ng'ombe Sarvopaniṣado. Na ndio kiini cha Upaniṣad zote na imewasilishwa kama ng'ombe. Na kwa kuwa Bwana ni mtaalam katika maswala ya kuhusu ng'ombe. Anamkamua ng'ombe. Na pārtho vatsaḥ. Na Arjuna ni kama vile ndama. Na su-dhīr bhoktā.. Na wasomi na waja wanafaa kunywa hayo maziwa. Su-dhīr bhoktā dugdhaṁ gītāmṛtaṁ mahat. Nta, maziwa ya Bhagavad-gītā, ni ya waja ambao ni wasomi.

ekaṁ śāstraṁ devakī-putra-gītam
eko devo devakī-putra ev
eko mantras tasya nāmāni yāni
karmāpy ekaṁ tasya devasya sevā
(Gītā-māhātmya 7)

Sasa dunia inafaa kujifunza kutoka kwa Bhagavad-gītā, funzo. Evaṁ śāstraṁ devakī-putra-gītam. Kuna andiko moja tu, andiko moja la dunia nzima, kwa atu wa dunia nzima, na hiyo ni Bhagavad-gītā hii. Devo devakī-putra eva. Na kuna Mungu mmoja wa dunia nzima amabaye ni Śrī Kṛṣṇa. Na eko mantras tasya nāmāni. Na nyimbo moja, mantra, nyimbo moja tu, ombi moja, au nyimbo moja, ni kukariri jina lake, Hare Kṛṣṇa Hare Kṛṣṇa Kṛṣṇa Kṛṣṇa Hare Hare, Hare Rāma Hare Rāma Rāma Rāma Hare Hare. Eko mantras tasya nāmāni yāni karmāpy ekaṁ tasya devasya sevā. Na kuna kazi moja tu, amabayo ni kuhudumia Mwenyezi Mungu. Ikiwa mtu atajifunza kutoka kwa Bhagavad-gītā, basi watu wana wasi wasi mwingi kupata dini, Mungu mmoja, andiko moja na kitendo kimoja maishani. Imedokezwa kwenye Bhagavad-gītā. Kuwa yeye, Mungu mmoja ni Krishna. Krishna sio Mungu wa wakidini. Krishna kutoka kwa jina la Krishna... Krishna inamaanisha, kamatulivyo eleza hapo awali. Krishna inamaanisha radhi kuu.