SW/Prabhupada 1079 - Bhagavad-gita ni Kitabu cha kiroho ambacho mtu anafaa kusoma kwa maakini sana

From Vanipedia
Jump to: navigation, search
Go-previous.png Previous Page - Video 1078
Next Page - Video 1080 Go-next.png

Bhagavad-gita ni Kitabu cha kiroho ambacho mtu anafaa kusoma kwa maakini sana - Prabhupāda 1079


660219-20 - Lecture BG Introduction - New York

Kuskiza hii Bhagavad-gītā au Śrīmad-Bhāgavatam kutoka kwa mtu aliye kamilika, hita mfunza mtu kumfikiria Mwenyezi Mungu masaa ishirini na nne, amabayo hatimaye ita msababisha mtu kumkumbuka Mwenyezi Mungu, na baada ya kuwacha mwili wake, akuwa na mwili wa kiroho, mwili wa kiroho, ambayo inamtosha kushirikiana na Bwana. Bwana kwa hivyo anasema,

abhyāsa-yoga-yuktena
cetasā nānya-gāminā
paramaṁ puruṣaṁ divyaṁ
yāti pārthānucintayan
(BG 8.8)

Anucintayan, kumfikiria Yeye tu wakati wote. Sia swala gumu. Mtu lazima ajifunze njia hii kutoka kwa mtu aliye na uzoefu katika swala hili. Tad vijñānārthaṁ sa gurum evābhigacchet (MU 1.2.12). Mtu anapaswa kumwedea mtu amabaye tayari yuko kwenye njia hii. Kwa hivyo abhyāsa-yoga-yuktena. Hii inaitwa abhyāsa-yoga, kujifunza. Abhyāsa...Jinsi ya kumkumbuka Bwana wakati wote. Cetasā nānya-gāminā. Alkili wakati wote inaruka huku nakule Kwa hivyo mtu lazima ajifunze kumakinisha akili kwenye umbo la Mwenyezi Mungu Śrī Kṛṣṇa wakati wote, aua kwenye sauti, jina lake ambayo ime rahisishwa. Badala ya kumakinisha akili- akili yangu inaweza kuhangaika sana, kwenda huku na kule, lakini naweza kumakinisha sikio langu kwenye mtetemo wa sauti ya Krishna, na hiyo inaweza kunisaidia pia. Iyo pia ni abhyāsa-yoga. Cetasā nānya-gāminā paramaṁ puruṣaṁ divyaṁ. Paramaṁ puruṣa, yule Mwenyezi Mungu alaiye kwenye ufalme wa kiroho, kwenye mbingu ya kiroho, mtu anaweza kumfikia, anucintayan, kufikiria wakati wote. Kwa hivyo njia hizi zote zimetajwa kwenye Bhagavad-gītā, na hakuna kizuizi kwa yeyote. sio ati kikundi fulani cha watu wanaweza kumfikia. Kumfikiria Bwana Krishna inawezekana, kumsikiza Bwana Krishna kunawezekana kwa kila mmoja. Na Bwana anasema kwenye Bhagavad-gītā,

māṁ hi pārtha vyapāśritya
ye 'pi syuḥ pāpa-yonayaḥ
striyo vaiśyās tathā śūdrās
te 'pi yānti parāṁ gatim
(BG 9.32)
kiṁ punar brāhmaṇāḥ puṇyā
bhaktā rājarṣayas tathā
anityam asukhaṁ lokam
imaṁ prāpya bhajasva mām
(BG 9.33)

Bwana anasema kuwa hata mwanadamu aliye kwenye kiwango cha chini cha maisha, au mwanamke aliye anguka kitabia au mwana biashara au mfanyi kazi... Kundi la wana biashara, wafanyi kazi na mwanamke, wanahesabiwa kuwa kwenye kundi moja kwa sababu akili haijafafanuka kamili. Lakini Bwana anasema, hao pia au walio chini kuwaliko, māṁ hi pārtha vyapāśritya ye 'pi syuḥ (BG 9.32), sio hao pekee au walio chini yao, au mtu yeyote. Haijalishi ni nani, mtu yeyote amabaye anakubali kanuni hii ya bhakti-yoga na anamkubali Mwenyezi Mungu kuwa jumla yote ya maisha, lengo kuu, lengo kuu la maisha... Māṁ hi pārtha vyapāśritya ye 'pi syuḥ, te 'pi yānti parāṁ gatim. parāṁ gatim iyo kwenye ufalme wa kiroho na mbingu ya kiroho, inaweza kufikwa na mtuyeyote. Ila mtu ajifunze mfumo huo. Mfumo umedokezewa vizuri sana kwenye Bhagavad-gītā na mtu anaweza kuifuta na kukamilisha maisha yake na kupata suluhisho daima la maisha. Hiyo ndio jumla yote ya Bhagavad-gītā. Kwa hivyo kiitimisho ni kwa Bhagavad-gītā ni kitabu cha kiroho ambacho kinafaa kusomwa kwa maakini. Gītā-śāstram idaṁ puṇyaṁ yaḥ paṭhet prayataḥ pumān. Na matokeo itakuwa, akifuata mazfunzo kwa maakini, basi anaweza kuokolewa kwenye taabu za dunia, wasi wasi wote maishani. Bhaya-śokādi-varjitaḥ (Gītā-māhātmya 1). Woga wote maishani, na pia atapata maisha ya kiroho kwenye maisha yake ijayo.

gītādhyāyana-śīlasya
prāṇāyama-parasya ca
naiva santi hi pāpāni
pūrva-janma-kṛtāni ca
(Gītā-māhātmya 2)

Kwa hivyo manufaa ni kuwa mtu akisoma Bhagavad-gītā, kwa dhati na umakinifu basi kwa neema ya Bwana, matokeo ya dhambi zake hazita tendeka kwake.