SW/Prabhupada 1070 - Dini ya milele ya Kiumbe ni kutoa huduma

From Vanipedia
Jump to: navigation, search
Go-previous.png Previous Page - Video 1069
Next Page - Video 1071 Go-next.png

Rendering of Service is the Eternal Religion of the Living Being - Prabhupāda 1070


660219-20 - Lecture BG Introduction - New York

Kulingana na mtazamo wa amwali wa sanātana-dharma, tunaweza kuelewa maana ya dini kutoka kwenye mizizi ya lugha ya Sanskrit. Inamaanisha, kile kitu ambacho kiko daima kwenye kitu fulanani. Na kama tulivyo sema hapo awali, tunapo on'gea kuhusu moto vile vile tunahitimisha kuwa, joto na mwanga pio zipo ndani ya moto. Bila joto au mwanga, jina moto haina maana. Vile vile lazima tutafute viungo fulani vya kiumbe ambavyo daima viko ndani ya roho yake. Tabia daima ya kiumbe ni kile kiungo ambacho kiko daima ndani ya roho yake, na kiungo hicho ndiyo dini daima ya kiumbe huyo. Wakati Sanātana Gosvāmī alimuuliza Bwana Caitanya Mahāprabhu kuhusu svarūpa— tulisha jadili kuhusu svarūpa ya viumbe vyote- Bwana akajibu kuwa svarūpa au cheo halisi cha kimbe, ni kutoa huduma kwa Mwenyezi Mungu. Lakini tukichambua haya maneno ya Bwana Chaitanya, tunaweza kuona kuwa kila kiumbe kina shiriki katika kazi hiyo ya kutoa huduma kwa kiumbe kingine daima. Kiumbe kingine kwa kiwango fulani, na kwa kufanya hivyo, anafurahia maisha. Mnyama ana mhudumia binaadam, na mjakazi ana mhudumia bwana wake, A ina hudumia B, B ina hudumia C bwana na C ina hudumia D bwana na kadhalika. Katika hali fulani tunaweza kuona kuwa mtu ana mhudumia rafiki yake na mama ana mhudumia mwanake au bibi ana mhudumia bwanake au bwana anam hudumia bibi yake tukiendelea kutafuta kwa hiyo roho, itaonekana kuwa hakuana mahali katika mazingira ya binaadam vitendo vya huduma havionekani. Mwana siasa anatoa maoni yake kwa umma na kuwashawishi wapigaji kura kuhusu viwango vya huduma yake. Kisha mpigaji kura anampa kura yake na kutarajia kuwa mwana siasa huyo atapeana huduma kwa jamii. Mchuruzi ana mhudumia mteja na fundi ana mhudumia bepari. Bepari ana hudumia familia yake, na familia yake ina mhudumia mkuu wa familia hiyo. Kwa njia hii tunaweza kuona kuwa hakuna kiumbe yeyote ambaye ameachwa nyuma, katika kazi ya kutoa huduma kwa kiumbe mwingine, kwa hivyo tunaweza hitimisha kuwa huduma ni kitu ambacho ni kina andamana na kiube daima, Kwa hivyo bila wasi wasi, inaweza kuhitimishwa kuwa utowaji wa huduma wa kiumbe ni yake dini daima. Wakati mtu anatangaza kuwa yeye ni wa imani fulani kulingana na wakati na mazingara ya kuzaliwa, alafu anadai kuwa yeye ni Muhindi, Muislamu, Mukristo, Mbuda au dhehebu lingine lolote, au dhehebu nyingine ndogo, maono hayo yote sio sanātana-dharma kamwe. Muhindi anaweza kubadili imani yake na kuwa Muislamu, au Muislamu anaweza kubadili imani yake na kuwa Muhindi au Mkristo, nakadhalika., kwa hali hizo zote, mbadiliko huo wa imani ya kidini haiweza kubadilisha msimamo wa mtu kutoa huduma kwa mwingine. Katika hali zote Muhindi au Muislamu au Mkristo ni mtumishi wa mtu fulani, kwa hivyo madai ya kuwa na imani fulani sio sanātana-dharma kamwe, ila mwandama daima wa kiumbe ni kutoa huduma, iyo ndiyo sanātana-dharma. Kwa hivyo tuna uhusiano wa ki huduma na Mwenyrzi Mungu. Mwenyezi Mungu mdiye mfaidi mkuu, na sisi viumbe ni watumishi wake daima. Tumeumbwa kwa faida zake, na tukishiriki katika faida hiyo daima na Mwenyezi Mungu, tutafurahia. kama tulivyo eleza hapo awali kuwa kiungo chochote cha mwili, mikono, miguu, vidole au kiungo chochote kikiwa kivyake hakiwezi kufurahia bila kushirikiana na tumbo, vile vile, kiumbe hawezi kufurahia kamwe bila kutoa huduma yake ya kumpendeza Mwenyezi Mungu. Ibada kwa miungu imekataliwa kwenye Bhagavad-gītā kwa sababu... Imesemekana kwenye (Bhagavad-gītā) sura ya saba, mstali wa ishirini, Bwana anasema, kāmais tais tair hṛta-jñānāḥ prapadyante 'nya-devatāḥ. Kāmais tais tair hṛta-jñānāḥ. Wale wanao ongozwa na tamaa, ndiyo wanao abudu miungu badala ya Mwenyezi Mungu, Kṛṣṇa.