SW/Prabhupada 1071 - Tukishirikiana na Bwana, pia sisi tutakuwa na furaha

From Vanipedia
Jump to: navigation, search
Go-previous.png Previous Page - Video 1070
Next Page - Video 1072 Go-next.png

If We Associate with The Lord, Cooperate with Him, Then also We Become Happy - Prabhupāda 1071


660219-20 - Lecture BG Introduction - New York

Tukumbuke pia kuwa "Kṛṣṇa" haimaanishi jina la dhehebu fulani. "Kṛṣṇa" inamaanisha radhi ilio kuu. Imetibitishwa kuwa Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kuhifadhi radhi zote. Sote tunatafuta furaha. Ānandamayo 'bhyāsāt (Vedānta-sūtra 1.1.12). Kwa sababu tumejawa na fahamu, viumbe vyote pamoja na Bwana, fahamu zetu zinatafuta furaha. Furaha. Bwana pia anafuraha daima, na tukishirikiana na Bwana, tukichukua nafasi katika ushirikiano wake, basi pia sisi tutakuwa na furaha. Bwana anashuka duniani kuonyesha visa vyake vilivyo jawa na furaha kule Vṛndāvana. Wakati Bwana Śrī Kṛṣṇa alikuwa Vṛndāvana, vitendo Vyake na rafiki zake, na vijakazi wake, na wakaazi wa Vṛndāvana pamoja na kazi yake ya kulinda ng'ombe utotoni, na visa hivi vyote vya Bwana Kṛṣṇa vilijawa na furaha. Na wakaazi wote wa Vṛndāvana, walikuwa wanamtafuta yeye. Hawaku fahamu lolote isipokuwa Kṛṣṇa. Hata Bwana Kṛṣṇa alimkataza babake, Nanda Mahārāja kumuabudu mfalme Indra, kwa sababu ilitaka kuzindua ya kuwa watu hawahitaji kuabudu mfalme yeyote ila Mwenyezi Mungu. Kwa sababu lengo la maisha ni kurudi nyumbani kwenye makaazi ya Mwenyezi Mungu. Makaazi ya Bwana Kṛṣṇa imeelezwa kwenye Bhagavad-gītā, sura ya kumi na tano, mstari wa sita,

na tad bhāsayate sūryo
na śaśāṅko na pāvakaḥ
yad gatvā na nivartante
tad dhāma paramaṁ mama
(BG 15.6).

Maelezo ya mbingu daima... Kwa sababu tuna mtazamo kidunia wa mbingu, tunapo ongea kuhusu mbigu, tunafikiria kuhusu mbigu iliyo na jua, mwezi, nyota na kadhalika. Lakini Bwana ansema kuwa mbingu iliyo daima, haihitaji jua. Na tad bhāsayate sūryo na śaśāṅko na pāvakaḥ (BG 15.6). Wala mbingu haihitaji mwezi. Na pāvakaḥ inamaanisha kuwa hakuna haja ya stima au moto kuangazwa kwa sababu mbingu ya kiroho tayari imeangazwa na brahma-jyotir. Brahmajyoti, yasya prabhā (BS 5.40), nuru za makaazi makuu. Siki hizi watu wanapo jaribu kufikia sayari zengine, sio vigumu kuelewa makaazi ya Mwenyezi Mungu. Makaazi yake iko kwenye mbingu ya kiroho inajulikana kama Goloka. Imeelezwa vizuri sana kwenye Brahmā-saṁhitā, goloka eva nivasaty akhilātma-bhūtaḥ (BS 5.37). Ingawa Bwana ananakaa daima kwenye makaazi yake Goloka, bado yu akhilātma-bhūtaḥ, pia anaweza kukaribiwa kutka hapa. Na kwa hivyo Bwana anakuja ili adhiirishe umbo lake la sac-cid-ānanda-vigraha (BS 5.1), ili tusidhanie. Hakuna haja ya kudhania.