SW/Prabhupada 1078 - Kwa kuzama katika mafikira ya Bwana kwa akili na nia, masaa ishirini na nne

From Vanipedia
Jump to: navigation, search
Go-previous.png Previous Page - Video 1077
Next Page - Video 1079 Go-next.png

Absorbed Both By The Mind and Intelligence Twenty-four Hours Thinking of the Lord - Prabhupāda 1078


660219-20 - Lecture BG Introduction - New York

Wakati una hisia kuu ya mapenzi kwa Mwenyezi Mungu, basi inawezekana tutaendalea kufanya kazi zetu, na wakati huo huo tumkumbuke Bwana. Kwa hivyo ni lazima tukuze hali hiyo. Kama vile Arjuna waki wote alikuwa akimfikiria Bwana. Yeye, kati ya masaa ishirini na nne hakumsahau Krishna hata kwa sekunde moja. Mshiriki wa Krishna wakati wote. Na wakati huo huo, shujaa. Bwana Krishna hakumshauri Arjuna kuwacha vita vyake, nenda msituni, nenda kule Himalaya na utafakri. Wakati mfumo wa yoga ulishauriwa kwa Arjuna, Arjuna alikataa kuwa "Mfumo huu siuwezi." Alafu Bwana akasema yoginām api sarveṣāṁ mad-gatenāntarātmanā (BG 6.47). Mad-gatenāntarātmanā śraddhāvān bhajate yo māṁ sa me yuktatamo mataḥ. Kwa hivyo anaye mfikiria Mwenyezi Mungu wakati wote ndiye yogi mkuu, yeye ndiye jñānī mkuu, na pia wakati huo huo ndiye mja mkuu. Bwana anahimiza kuwa tasmāt sarveṣu kāleṣu mām anusmara yudhya ca (BG 8.7). "Kama kṣatriya (shujaa) hauwezi kuacha kazi yako ya kupigana. Lazima upigane. Kwa hivyo wakati huo huo, ukijifunza kunikumbuka wakati wote, basi itawezekana," anta-kāle ca mām eva smaran (BG 8.5), "basi itawezekana kunikumbuka wakati wa kifo chako pia." Mayy arpita-mano-buddhir mām evaiṣyasy asaṁśayaḥ. Tena anasema kuwa hamna shaka. Ikiwa mtu amejisajili katika huduma ya Bwana kabisa, kwenye huduma kuu ya mapenzi kwa Bwana , mayy arpita-mano-buddhir (BG 8.7). Kwa sababu hatufanyi kazi kwa kutumia mwili wetu kamwe. Tuna fanya kazi kwa nia na fikra zetu. Kwa hivyo ikiwa nia na fikra zetu zina husika wakati wote kwenye mawazo ya Mwenyezi Mungu, basi kama kawaida fahamu zetu pia zitahusika kwenye huduma ya Bwana. Iyo ndiyo siri ya Bhagavad-gītā. Mtu lazima ajifunze sanaa hii, vile ambavyo anaweza kuzama kwa nia pamoja na fikra, masaa ishirini na nne akimfikiria Bwana. Na hiyo itamsaidia kujisafirisha kwenye ufalme wa Mungu au kwenye mazingira ya kiroho baada ya kuacha mwili huu. Wana sayansi wa kisasa, wanapigana wenyewe miaka nenda rundi kufikia sayari ya mwezi, na mpaka sasa hawajafika. Lakini hapa kwenye Bhagavad-gītā, kuna mpendekezo. Tuseme mtu aishi kwa miaka hamsini ijayo na a... Kwa hivyo hakuna atakayejiinua katika maswala ya kiroho kwa miaka hamsini. Iyo ni wazo zuri sana. Lakini hata kwa miaka kumi au tano mtu ajaribu kujifunza, mayy arpita-mano-buddhir (BG 8.7)... ni swala tu la zoezi. Na zoezi hiyo inaweza ku rahisishwa sana kwa njia ya ibada, Śravaṇaṁ. njia rahisi sana ni kusikia

śravaṇaṁ kīrtanaṁ viṣṇoḥ
smaraṇaṁ pāda-sevanam
arcanaṁ vandanaṁ dāsyaṁ
sakhyam ātma-nivedanam
(SB 7.5.23)

Hizi njia tisa. Kwa hivyo njia rahisi ni kusikia tu.